Zinazobamba

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA KALI WANAOFANYA UVUVI HARAFU,WAZIRI MPINA ATOA NENO WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO WA WIOMSA,SOMA HAPO KUJUA


Pichani ni Mkurugenzi wa wa Taasisi ya Utafiti wa Madawa ya Binadamu nchini,Profesa Yunus Mgaya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Kongamato la siku nne la wanasayansi wa Bahari kutoka Ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi(WIOMSA),
 NA KAROLI VINSENT
Serikali imesema inaendelea kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kusimamia sheria za uvuvi ili kudhibiti vitendo vya uvuvi halamu ambavyo vinavyosababisha kutoweka kwa baadhi ya viumbe vya majini.
Hayo yamesema leo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina alipokuwa anamwakilisha Makamu wa Rais Samia Suluhu katika Kongamato la siku nne la wanasayansi wa Bahari kutoka Ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi(WIOMSA), kwa ajili ya kujadili masuala mbali mbali yanayohusu shughuli za Baharini..

Amesema kwamba baadhi ya viumbe vya baharini vimekuwa vikitoweka kutokana na shughuli za kibinadamu.
“Shughuli za Uvuvi haramu,utililishaji wa maji ya sumu kutoka viwandani haya yote ynachangia kupotea kwa viumbe baharini,na ndio maana tumekutana kwenye mkutano huu kujadili ili tuweze kuondokana na tatizo hili”Amesema Mpina.
Amesema katika mkutano huo wadau watajadili mikakati ya namna ya kusaidia kuondokana na changamoto za uvui haramu pamoja utumiaji wa utilishaji wa kemikali hizo akitolea mfano kemikali hatari ya  Zebaki.
“Serikali tutachukua haya mapendezeko yote yatakayotolewa na wadau hawa ili ziweze kuchukuliwa kuondokana na hizi changamoto”amesema Mpina.

Kwa wake Mkurugenzi wa wa Taasisi ya Utafiti wa Madawa ya Binadamu nchini,Profesa Yunus Mgaya ameishauri serikali kusimamia sheria zake ili kuweza kudhibiti vitendo haramu vya uvuvi.
“Sheria zipo naishauri serikali itilie mkazo wa nguvu kwenye sheria za uvuvi haramu ambapo itachangia kupunguza vitendo hivi”ameishauri Profesa Mgaya.
Mkutano huo wa siku nne umeanza leo  Octoba 30 na unatarajua kumalizika Novemba 4 mwaka huu,ambao umekutanisha wadau mbali mbali kutoka nchi tofauti .