Zinazobamba

NECTA YATANGAZA MATOKEO YA DARASA LA SABA LEO,SOMA HAPO KUJUA


Mkurugenzi Mtendaji wa NECTA Dk. Charles Msonde
BARAZA la Mitihani nchini (NECTA) limesema kiwango cha ufaulu katika mtihani wa darasa la saba uliofanyika Septemba 6 hadi 7 mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 2.40 ukilinganisha na mwaka jana.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa NECTA Dk. Charles Msonde akitangaza  matokeo hayo, amesema watahiniwa  662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani wamefaulu kwa kupata alama 100 au Zaidi kati ya alama 250.

Kati yao Wasichana ni  341,020 ambao ni sawa na asilimia 70.93 huku wavulana ni  321,015 sawa na asilimia 74.80.


Dk. Msonde amesema pia katika takwimu za matokeo zinaonyesha ufahulu katika masomo ya Kiswahili,Kiingereza  na Hisabati umepanda  kwa asilimia 4.25   ikilinganishwa  na mwaka 2016.

“Watahiniwa wamefaulu  Zaidi katika  somo la Kiswahili  ambapo ufaulu ni asilimia 86.86 na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini Zaidi ni English Language lenye  ufaulu wa asilimia 40.30,”amesema Dkt Msonde.

Hata hivyo Dk. Msonde ameiitaja mikoa iliyoongoza kitaifa ni Dar eSalaam,Geita,Kagera,Iringa,Kilimanjaro,Njombe, Arusha, Mwanza, Katavi, Tabora.

Kuhusu wanafunzi 10  bora kitaifa waliofanya vizuri kwenye mtihani huo ni Ibrahim Shaban kutoka Shule ya Tusiime iliyopo mkoani Dar es Salaam, Kadidi Mkama Kaddi kutoka shule ya Paradise iliyopo mkoani Geita,Mahir Ally Muhamed kutoka shule Feza iliyopo Mkoani Dar es Salaam,Mbarak Faraj kutoka shule hiyo hiyo ya Feza,

Dk, Msonde amewataja wengine waliofanya vizuri ni Philimon Damas kutoka shule ya  St.Achileus iliyopo mkoani Kagera ,Huruma Godfrey kutoka shule  Mwanga iliyopo Mkoani Kagera ,Hamza Azael Almas kutoka shule ya Azina  iliyopo Mkoani Dar es Salaam,Gibbons  Roy Fountain of Joy iliyopo Dar es Salaam,pamoja Erastus Joseph kutoka  shule St Peter Claver iliyopo Mkoani Kagera.


 Pamoja na hayo Dk Msonde  Baraza hilo limetoa wito kwa Maafisa  elimu wa Mkoa ,Halmashauri,Manispaa ,wadhibiti Ubora wa Elimu,wamiliki wa shule,Walimu wahakikishe ufundishaji na ujifunzaji unaimarishwa  katika  masomo yote shuleni ili kuwawezesha wanafunzi kupata umahiri unaotarajiwa.