Zinazobamba

VETA na Ujermani waingia makubaliano kutoa mafunzo ya ujuzi wa kilimo kusaidia vijana kupata ajira


MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeingia makubaliano na Serikali ya Ujerumani katika kutoa mafunzo ya kilimo kwa vijana  ili kuwaongezea ujuzi wakuwasaidia kupata ajira.


Utiaji saini makubaliano hayo ulifanyika  jana jijini Dar es Salaam baina  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Moshi Kabengwe na Mkurugenzi Mkuu wa Mradi huo Reiner Nolten wenye lengo la kutoa mafunzo ya kuongeza uzalishaji ya kilimo nchini.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Kabengwe alisema mafunzo hayo yatasaidia kuongeza ujuzi kwa vijana katika masomo na kuwa vizuri katika elimu ya ufundi ambayo itawawezesha kupata ajira kwa urahisi.

“Mradi huu unamanufaa sana kwa vijana, utawasaidia kuwapa ujuzi na kuweza kupata ajira, lakini pia kuendeleza nchi kiuchumi,” alisema Kabangwe.

Balozi wa Ujermani nchini Defflef Waechoter ambaye alikuwa shuhuda wakati wakutiliana saini, alisema Ujermani imeendelea kiuchumi kwa kuwekeza katika mafunzo hayo ya kilimo hali ambayo imekuwa ikiwaingizia fedha nyingi.
Alisema kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Ujermani wataendelea kushitikiana na Serikali pamoja na Wananchi wa Tanzania kwa ajili ya maendeleo.

Mkurugenzi wa Mafunzo ya VETA Leah Lukindo Mfumo wa Wanagenzi umeiletea maendeleo nchi ya Ujermani hivyo kwa kushirikiana nao wataweza kuleta mapinduzi ya maendeleo nchini hususani katika sekta ya kilimo.

Aidha alisema wamekuwa wakiendesha mafunzo kwa vijana huku wakishirikiana na waajiri, kutokana na hali hiyo wanafunzi wanapomaliza mafunzo wanakuwa wameshajua hali ya mazingira kazi hivyo kuwa rahisi kuajiliwa.





Na