Zinazobamba

MBUNGE KUBENEA ALIA NA WANAFUNZI KUJAZANA MASHULENI,SOMA HAPO KUJUA

SAED Kubenea Mbunge wa Ubungo jijini Dar es Salaama, amesikitishwa na kuwapo msongamano wa wanafunzi katika shule ya Msingi Kawawa, anaandika Faki Sosi.
Msongamano huo unatokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo.
Kubena akiwa katika shule hiyo iliyopo kata ya Mabibo, alishuhudia msongamano wa wanafunzi shuleni hapo ambapo wanafunzi 3100 ambao wanatumia vyumba 32 wakati mahitaji ni vyumba 64.
Mbunge huyo alifika katika shule hiyo baada ya kuombwa na uongozi wa kamati ya shule kuja kuangalia sehemu litakapojengwa jengo la utawala wa shule hiyo na kusikiliza kero mbalimbali.
Mbunge huyo akizungumza na kamati ya shule, aliahidi kuchangia gharama za chakula kwa ajili ya wafanyakazi watakaofyatua matofali ili kurahisha ujenzi wa jengo hilo.


Wakati huo huo Kubenea ameushari uongozi wa shule kuangalia uwezekano wa kujenga majengo ya ghorofa ili kukabaliana na uhaba wa maeneo.
Katika ziara hiyo, Kubenea alipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi wa darasa la saba wanaojiandaa na mitihani yao ya taifa na kuahidi kuwalipia ada watoto watatu wa kwanza watakaofaulu mitihani yao.