SHEIKH WA MKOA: TUMUENZI IMAM KHOMEINI KWA KUKITHIRISHA UPENDO BAINA YETU, KIONGOZI WA KANISA APENDEZWA NA MATENDO YA KHOMEINI
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa, amesema Imaam Khomeini anapaswa
kuenziwa kwa vitendo hususani kuongeza jitihada za kupendana baina yetu,
kuthamini wengne kwani kufanya hivyo kutasaidia kustawisha Amani iliyopo
nchini. Pia amewasihi viongozi wa dini na vijana kujitoa kama Imam
Khomein (r.a) ambaye alijitoa kwa ajili ya watu wote ulimwenguni.
Wito
huo ulitolewa jana Dar es Saalam wakati wa semina iliyozungumzia mchango
wa Imam Khomein (r.a) katika ulimwengu, ambayo iliyofanyika katika Masjid
Ghadir, Kigogo Post Dar es Salaam.
Kiongozi mkuu wa Waislam Shia Ithna Asheriya Sheikh Hemed Jalala akiongea kwa msisitizo kuhusu umoja na msikamano kwa dini zote |
Sheikh Alhad Mussa amesema Imam
Khomein (r.a) alijitoa kwa ajili ya watu wote ulimwenguni, hakujitoa kwa
ajili ya waislamu pekee, na wala hakujitoa kwa mashia pekee, bali
amejitoa kwa kuhakikisha wanaadamu wanapata haki zao, wanyonge wanapata
haki zao, na madhalimu hawana nafasi katika jamii.
|
Imam Khomein alikuwa ni mtu wa watu, alikuwa anapenda haki, alikuwa
anapenda usawa na alikuwa anawatetea watu wanaonyonywa pamoja na
kuwatumikia watu kwadhati,
“Nashukuru sana kwasababu ninajifunza mengi ndani ya dini ya
Kiislamu,hata miezi iliyopita nilimkaribisha sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam Sheikh Alhad Mussa katika kanisani kwangu na nikampatia Ibada,
ili ahutubie, waumini walifurahi sana,
Sisi Viogozi wa Dini tukiwa tunaonyesha ushirikiano baina yaViongozi wa
Kikrito na Viongozi wa Kiislamu tunazidi kufungua nafasi zaidi ya
Upendo, Mahusiano mema kati ya Udugu wa Wakristo na Waislamu
Nae Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed
Jalala amesema kuwa Uislam unafunza kukaa vizuri na watu wote, unafunza
huruma, unafunza amani na upendo kwa watu wote.
Aidha Sheikh Jalala amesema kuwa Uismau hauko dhidi ya asiyekuwa Mwislamu badi Uislamu upo dhidi ya Mtu yoyote amabe ni Dhalimu