SAKATA LA POLISI KUMUUA IMAMU SALUM,FAMILIA YAKE YACHACHAMAA,SOMA HAPO KUJUA

NA KAROLI VINSENT
FAMILIA ya Marehemu Imamu Salum Mohammed Almasi aliyeuwawa na Jeshi la Polisi jijini kwa kupigwa risasi Dar es Salaam kwa kudaiwa kuwa ni Jambazi,Familia hiyo imeibuka tena huku ikitaka serikali kuunda tume itakayochunguza kifo cha ndugu yao huyo.
Pia Familia hiyo imesema itaendelea kususia kuzika Mwili wa Marehemu Imam Salum mpaka pale jeshi la Polisi litakapokubali kumuua kimakosa.
Hayo yamesema leo Jijini Dar es Salaam na Msemaji wa Familiya ya marehemu,Mohamed Abdulrahman wakati wa mkutano na waandishi wa habari,ambapo amesema wanaitaka serikali kuunda tume kuchunguza tukio la kuuawa ndugu yao ili ukweli upatikane kwani wanaamini ndugu yao huyo hakuwa jambazi kama ilivyoripotiwa na aliyekuwa Kamishna wa Polisi Kanda Maalumya Dar es Salaam,Simmon Sirro/
“Tunaiomba serikali kuingilia suala hili kwa kuunda tume itakayochunguza tukio hili,hatukubaliani na maelezo ya jeshi la polisi kuwa ndugu yetu alikuwa jambazi,sio kweli kwani Marehemu hajawai kuhusika na vitendo vyovyote viovu kwa jamii,kwahiyo tunaiomba serikali iunde kamati itayochunguza kifo cha ndugu yetu”amesema Abdulrahman.
Abdulrahman ,amesema Familiya itaendelea kususia mwili wa marehemu kwa kutokwenda kuuzika mpaka pale Jeshi la Polisi litakapokubali kuwa Marehemu salum hakuwa jambazi.
“Kwa mazingira ya utata ya kifo cha ndugu yetu tunaendelea kususia mwili ya marehemu mpaka pale Jeshi la polisi likikubali kuwa limehusika sisi tutachukua tutakwenda kuuzika,”
Amesema endapo kilio hicho cha serikali hakitasikilizwa kwa kutoundwa tume itakayochunguza kifo hicho au jeshi la Polisi kutoibuka hadharani na kukubali kumuua ndugu yao huyo kimakosa,basi wataenda Mahakamani
“Na kama Polisi wakikataa kukubali kosa la kumuua ndugu yetu kimakosa,au kamati kama haitaundwa basi sisi tutakimbilia mahakamani ili ukweli upatikane”amesema Abdulrahman.
Hata hivyo, Abdulrahman amesema maelezo yanayotolewa na Jeshi la polisi kuwa tarehe 14 Mei, 2017, Salum Muhamed Almasi aliuwawa kwa kupigwa risasi na Polisi majira ya saa 3:00, na saa 4:00, asubuhi eneo la Kurasini Dar es Salaam wakati akitaka kupora fedha milioni 350 za Benki ya CRDB hazina ukweli.
“Hata ukiangalia eneo la tukio alilouawa marehemu kunaonyesha polisi wanapotosha,anachosema Sirro kuwa Polisi walikuwa wakipambana na marehemu sio kweli kwani marehemu alikuwa upande wa mbali na tukio na hata marehemu hakuwa na silaha ambayo unaweza kusema labda alikuwa na mapambano na polisi.’’