Zinazobamba

Mkuu wa Mkoa Meck Sadiki na Majaji wawili Waandika barua kuacha kazi .......Rais Magufuli Aridhia

Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia maombi ya kuacha kazi kwa viongozi wafuatao;

1. Ndg. Saidi Meck Sadiki - Aliyekuwa mkuu Wa Mkoa wa Kilimanjaro.

2. Ndg. Aloysius Kibuuka Mujulizi - Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

3. Ndg. Upendo Hillary Msuya - Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 16 Mei, 2017 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inaeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli ameridhia maombi ya kuacha kazi kwa viongozi hao kuanzia tarehe 15 Mei, 2017.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
IKULU Dar es Salaam 
16 Mei, 2017