MKEMIA MKUU AFUNGUKA MAZITO,SOMAHAPO KUJUA
MkemiaMkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyere akizungumza na waandishi habari juu uingizaji Kemikali bashirifu ambazo zinafuata sheria iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam |
Hayo yamesemwa leo na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele wakati alipozungumza na wanahabari kuhusu kampuni ya Techno Net Scientific kukutwa na kemikali bashirifu bila usajili.
Amesema ofisi yake ilitoa usajili wa muda wa miaka miwili kwa kampuni hiyo ambao uliishia Aprili 30 mwaka 2016 lakini bado ikawa inaendelea na shughuli zake kinyume cha sheria.
Profesa Manyele alibainisha kuwa kampuni hiyo imebainika kwamba imekuwa ikiingiza kemikali nchini kwa kutumia njia za udanganyifu na vibali vya bandia.