Kampuni ya simu za mkononi ya Tecno imeandaa tafrija fupi iliyowakutanisha pamoja wateja wa simu za Tecno, wafanyakazi wa kampuni hiyo pamoja na wauzaji wa simu kwa jumla. Tafrija hiyo iliyofanyika usiku wa jana katika eneo la Dar Free Market jijini Dar es salaam na kupewa zawadi ya tiketi kwa wateja zaidi ya 170 kuweza kuangalia movie mpya kabsa katika ukumbi wa Century Cnemax.
Akiongea na waandishi wa habari meneja mahusiano wa kampuni hiyo bw. Eric Mkomoye alisema kuwa mara kwa mara Tecno imekuwa ikitoa zawadi kwa wateja wake. Hii ikiwa na lengo la kuwakutanisha pamoja na kuwa karibu na wateja wao ili kujua matatizo na changamoto wanazokuna nazo wateja wao.
|
Meneja Mahusiano wa kampuni ya Tecno Tanzania Bw. Eric Mkomoye akiongea na waandishi wa habari mapema jana jijini Dar es salaam |
Na kusisitiza kuwa kuna simu mpya kwa sasa inayoitwa Camon CX ambayo inafanya vizuri sokoni na ina ubora wa hali ya juu wakupiga picha na mega pix 16 kwa kila camera ya mbele na nyuma na ina flash 2 kwenye camera ya mbele na 4 camera ya nyuma.
|
Balozi wa Tecno Tanzania Tony Albert (T-bway) akiongea na waandishi wa habari akielezea ufanisi wa Camon CX |
|
Afisa huduma kwa wateja Christina Simbano akimkabidhi zawadi ya tiketi mmoja wa washindi Bw. David Msia |
|
Balozi waTecno Tanzania Tony Albert akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washindi baada ya kukabidhiwa tiketi zao Christina Christopher kushoto na David Msia kulia. |
|
Balozi wa Tecno Tz Tony Albert akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Tecno wakionyeshana kitu kwenye simu ya Camon CX |