Zinazobamba

WAMACHINGA WA MWENGE WAISOMA NAMBA,SOMAHAPO KUJUA


Jeshi la Polisi limetumia silaha za moto kuwatawanya wafanyabiashara katika eneo la Mwenge, wilayani Kinondoni leo.

Taharuki iliwakumba wakazi wa eneo hilo mara baada ya polisi hao kuanza kuwatanya wafanyabiashara hao waliofunga barabara wakishinikiza magari yaruhusiwe kupaki katika eneo hilo.

Inaelezwa kuwa polisi wamezuia watu  kupaki magari katika eneo hilo  hali iliyosababisha wafanyabiashara hao kutofungua biashara zao leo.

Mmoja wa wafanyabiashara na shuhuda wa tukio hilo, Musa Godwin alisema polisi walifika sokoni hapo saa12 asubuhi na kutawanya wafanyabiashara waliofunga barabara kuzuia polisi magari yasiegeshwe eneo hilo.

"Walifika hapa sokoni saa 12 asubuhi na baadhi ya watu walifunga njia ikasababisha polisi wapige risasi hewani, hadi sasa wanazunguka hapa kuzuia magari ambao ni wanunuaji wetu," alisema Godwin.