Zinazobamba

SAKATA LAMITUNGU YA GESI YA TANZANIA KUPIGWA STOP' KENYA,MBUNGE BASHE NAYE ATEMA CHECHE,SOMA HAPO KUJUA

Mbunge wa Nzega mjini, Hussein Mohamed Bashe amesikitishwa na Serikali ya Kenya kuweka zuio la kuingiza mitungi ya gesi inayotoka Tanzania kwa kusema ni vizuri nchi hiyo ikaheshimu mikataba ya 'East African Community (EAC)' .

Bashe amesema hayo baada ya serikali ya Kenya kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Andrew Kamau kupiga marufuku uagizaji wa gesi ya kupikia kutoka Tanzania kupitia mipaka ya nchi hiyo.

"Serikali ya Kenya imezuia gesi za matumizi ya nyumbani zinazotoka Tanzania kuingia Kenya ni vizuri Kenya ikaheshimu 'EAC treaty common'......Dar es salaam 'port and Cost' ya gesi inayotoka Tanzania ndiyo 'competetive edge' ya makampuni ya Tanzania dhidi ya yale ya Kenya uamuzi huu si sawa". Ameandika Bashe kupitia ukurasa wake wa twitter.
Serekali ya Kenya imezuia Gesi za matumizi ya nyumbani zinazotoka Tz kuingia Kenya ni vizuri Kenya ikaheshimu EAC treaty "Common mkt"

Quality ,Dar port and Cost ya Gesi inayotoka Tz ndo competitive edge ya Ma kampuni ya Tz dhidi ya Yale ya kenya uamuzi huu si sawa.

A