Zinazobamba

ORATA: MATUMAINI MAPYA KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI, ASSP MUSLIM AWATAKA KUPIGA KAZI



Mkuu wa operesheni kutoka kikosi cha Usalama barabarani Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Bw. Fortunatus Muslim akizungumza na Wanachama wa Taasisi inayopambana na vitendo vya ajali barabarani(ORATA), Katika semina ya siku moja iliyofanyika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) jijini Daresalaam.
http://www.itv.co.tz/media/image/musilimu.jpg
Mtendaji Mkuu wa ORATA,Doctor Kubin akifafanua jambo kwa Wanachama wa ORATA katika semina hiyo ya siku moja. Dr. Kubin amesema Taasisi ya ORATA ina kazi kuu mbili, moja ni kufanya tafiti mbalimbali zitakazowezesha watunga sera kuchukua hatua juu ya matatizo ya ajali pamoja na usafirishaji kwa ujumla wake, lakini kazi ya pili ni kuhakikisha taarifa ambazo zimefanyiwa tafiti zinawafikia wadau kwani kama taarifa hizo hazitawasilishwa zitakuwa hazija saidia Taifa

SEHEMU ya wadau wa ORATA wakifuatilia semina ya siku moja iliyofanyika Chuoni NIT, katika SEMINA hiyo wadau walipata fursa ya kufahamu mambo mbalimbali ikiwamo utafiti wa ajali (clash Investigation), usafirishaji wa mizigo hatarishi(Dangerous Goods like fuel)

Wadau wakifuatilia kwa makini. katika semina hiyo washiriki walifanikiwa kupata cheti, ikiwa ni ishara ya kupata mafunzo hayo
Na Mwandishi wetu.

Taasisi ya ORATA (Organization Against Transport Accidents) ni kama tumaini jipya kwa sekta ya usafirishaji. Kwa mujibu wa taarifa ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto nyingi za ajali za barabarani na hakuna tafiti za kitaalamu zilizofanywa zikiwa na lengo la kubaini sababu za kutokea kwake, na kama zimefanyika basi ni chache sana.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi,Mkuu wa operesheni kutoka kikosi cha Usalama barabarani Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Bw. Fortunatus Muslim amesema umoja wa ORATA utasaidia sana kurekebisha baadhi ya changamoto zinazojitokeza katika sekta ya usafirishaji.

Amesema kuanzishwa kwa Taasisi ya ORATA ni habari njema kwa taifa la Tanzania, ambapo anaamini kwa majukumu yao mawili ya kufanya tafiti na kuziwasilisha; kutaibua sera mpya ambazo hapo awali zilishindikana kuwepo kutokana na kutokuwepo watu wa kuonyesha sababu za kuwepo.