MIRADI YA GESI 68 MAJANGA,KAMATI YA PAC YALIA NA NEMC,SOMA HAPO KUJUA
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) jana waliibana Ofisi ya Makamu wa Rais baada ya kubaini miradi 68 ya sekta ya mafuta na gesi asilia haijakaguliwa na Baraza la Usimamizi wa Mazingira (Nemc).
Jana, PAC walikutana na Ofisi ya Makamu wa Rais kukagua ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuhusu ufanisi wa ofisi hiyo.
Mbunge wa Kilindi (CCM) Omari Kigua, alisema ripoti hiyo inaonyesha kati ya miradi 71 iliyopo katika sekta ya mafuta na gesi asilia ni miradi mitatu tu ndio iliyokaguliwa.
“Idara ya mazingira waliliona hili? Pia, hakuna coordination (ushirikiano) kati ya Nemc na sekta nyingine,” alisema.
Mbunge wa Sikonge (CCM), Joseph Kakunda alisema kabla ya Mwaka 2013, Nemc haikufanya ukaguzi katika miradi ya mafuta na gesi, lakini Mwaka 2014 ghafla iliibuka na kufanya ukaguzi.
“Hata walipofanya ukaguzi hawakuandaa taarifa kupeleka serikalini na idara ya mazingira pia haikuomba taarifa hiyo. Wanaongoza kwa kusafiri tu wanajulikana huko nje ya nchi,” alisema.
“Mimi nilifanya serikalini wanagawana mikutano tu hawana muda wa kufanya ukaguzi. Lakini, tunampongeza Rais (Dk John Magufuli) kwa kuzuia hili sijui tulikuwa tunaipeleka wapi nchi.”
Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM) Allan Kiula alisema kwa maelezo ya CAG inaonyesha kama wizara haikuwepo kabisa siku za nyuma.
“Kama hamkuwa na vifaa vya kufanya ukaguzi si mngetafuta watu wa kufanya (sub contract),” alisema.
Hata hivyo akijibu hoja hizo, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Nemc, Dk Vedast Makota alisema miradi inayofanyiwa ukaguzi ni miradi ambayo imeanza uzalishaji.
“Miradi iliyoanza uzalishaji kati ya hiyo 71 ni mitatu na ndiyo iliyokaguliwa na Nemc,” alisema.
Miongoni mwa miradi iliyokaguliwa ambayo ndiyo iliyoanza uzalishaji ni Songas na Mnazi Bay.
Alifafanua kuwa miradi yote kabla ya kuanzishwa husajiliwa na Nemc ili kufanya tathmini ya mazingira na kisha kupewa masharti ya kufuata wakati wa utekelezaji wa miradi husika.
Wakati huo huo, Mbunge wa Pangani (CCM), Jumaa Aweso alihoji ni lini Serikali itapeleka fedha ikiwa ni gawio lake katika utekelezaji wa mradi wa uhifadhi mazingira Pangani.
“Nashukuru sana kwa kuleta mradi huu lakini miradi hii inafanywa kwa ushirikiano kati ya wahisani wa maendeleo na Serikali. Wahisani wameshaleta fedha walizokuwa wakitakiwa kutoa katika mradi huo sasa ni lini fedha za Serikali zitafika,” alisema.
Akijibu hoja hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Profesa Faustin Kamuzora alisema ofisi hiyo katika mwaka wa fedha 2016/17 wamepewa asilimia tatu tu ya bajeti ya miradi ya maendeleo waliyotengewa.
Alisema fedha hiyo ilitumika kulipa mkandarasi ambaye alikuwa amekusudia kuwapeleka mahakamani.
“Lakini bado muda wa bajeti haujaisha kwa hiyo zitakapofika tutapeleka kwenye mradi wa Pangani,” alisema.
Akizungumzia hatua hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba alisema jumla ya miradi 71 ndiyo iliyosajiliwa na kupata cheti cha tathmini ya athari za mazingira.
“Kati ya miradi hiyo, mitatu ndiyo inayofanyika kazi na 68 haendeshwi,” alisema Makamba ambaye ni Mbunge wa Bumbuli (Tanga).

Reviewed by Unknown
on
14:57:00
Rating: 5