TIMU PROFESA LIPUMBA YAPATA PIGO ,MAHAKAMA YAAMURU ISIPEWE RUZUKU,SOMA HAPO KUJUA
Mahakama Kuu ya Tanzania, "Masijala ya Dar es Salaam" mbele ya Mhe Jaji Dyansobela katika shauri No. 28/2017 leo tarehe 31.03.2017 imetoa amri dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutotoa ruzuku ya Chama cha Wananchi CUF mpaka shauri la kupinga kitendo cha Msajili kutoa ruzuku kwa Lipumba litakapo malizika.
Mhe jaji alikubaliana na hoja za wakili Msomi Nassoro anayeiwakilisha Bodi ya Wadhamini ya CUF ili kuzuia fedha za umma (Ruzuku) zisichezewe.
Imetolewa na;
Mbarala Maharagande,
Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari,
The Civic United Front.