RC MAKONDA SASA AWAGEUKIA WAKAZI WA DARESALAAM
MKUU wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wakazi wa Jiji hilo kuwa tayari kubadilika
Akizungumza
na katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya maji Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Mhe. Paul Makonda amesema, katika kuadhimisha Wiki maji, Mkoa
wa Dar es Salaam umelenga kuwahamasisha na kuwaelimisha Wananchi,
Viongozi wa Serikali za Mitaa pamoja na Kamati za Maji kuhusu namna bora
ya usimamizi wa shughuli za maji katika maeneo yao ikiwemo na tarataibu
za umiliki wa visima.
Aidha
amesema kuwa miradi ya visima vya dharura katika maeneo yasiyo na maji
ya bomba ambapo ameeleza kuwa, DAWASA ina idadi ya visima 147, Manispaa
za mkoa zina visima 789 na Taasisi na Watu binafsi visima 600.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika
la Maji Safi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) Bw. Kiula Kingu
amesema kuwa, DAWASCO pamoja na DAWASA wamefanikiwa kuzuia upotevu wa
maji kwa kiasi kikubwa ambapo kwa mwaka jana ulikuwa ni asilimia 47 na mwaka huu umepungua na kufikia asilimia 38.6.
Naye
Meneja Mahusiano ya Jamii Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es
Salaam (DAWASA) Bi. Neli Msuya ameeleza kuwa, maeneo yote ya Dar es
Salaam yasiyo na mtandao wa maji yamekuwa yakitengenezewa ramani
(design) ili yawekewe mitandao hiyo ya maji ili maji yaweze kupatikana
kwa wakazi wa maeneo hayo.
Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “Majisafi na Majitaka-Punguza Uchafuzi yatumike kwa Ufanisi (Water and Waste Water-Reduce and Reuse).