JESHI LA POLISI LATAKA BODABODA DAR MWISHO SAA SITA USIKU,SOMA HAPO KUJUA
Jeshi ya Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
limetoa wito kwa madereva bodaboda katika Jijini la Dar es salaam, kuacha
kufanya shughuli hiyo ifikapo majira ya saa 6 usiku ili kupunguza uhalifu.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
Kamishna Simon Sirro, amesema kuwa jeshi hilo limebaini wahalifu wengi hutumia
mwanya katika muda huo kutenda uhalifu ikiwa ni pamoja na kuwadhuru waendesha
pikipiki.
Aidha, Kamanda Sirro, amesema, kuanzia Februari 18
hadi 23 Jeshi la Polisi Usalama Barabarani limefanikiwa kukusanya kiasi cha
shilingi milioni 460 kutokana na makosa mbalimbali ya barabarani pamoja na
kukamata pikipiki 1,280 kati ya hizo pikipiki 30 zimekamatwa kutokana na kupita
katika njia ya mabasi yaendayo haraka huku madereva 27 wakifikishwa mahakamani.
Kuhusu suala la dawa za kulevya, Sirro aliwaambia
waandishi wa habari jana kuwa mpaka sasa limefanikiwa kukamata jumla watuhumiwa
257 pamoja na kete za dawa za kulevya 1,526, puli 112 na misokoto ya bangi 247
kutokana na oparesheni inayoendelea.
Alisema baadhi ya watuhumiwa bado awajafikishwa
mahakamani kwani upelelezi bado haujakamilika na mara baada ya upelelezi
kukamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili