Zinazobamba

WANAWAKE NCHINI WANAONGOZA KUWA NA UGONJWA WA UKIMWI,SOMA RIPOTI YOTE HAPO,KWA KUBOFYA HAPO

http://www.tbc.go.tz/image.php?path=news_images/10124mhagama.jpg&width=600
NA KAROLI VINSENT
WAKATI ,Dunia leo Tarehe 1 Desemba, ikiazimisha siku ya ukimwi Duniani,inaelezwa kuwa Hali ya Maumbukizo ya ukimwi hapa nchini  kwa  upande wa Bara inaonyesha kuwa wanawake ndio kinara wa kwa maambukizo wa ugonjw
a wa ukimwi  kuriko wanaume.
Ambapo Tafiti inayonyesha asilimia 6.2 ya waathirika ni wanawake huku wanaume wakiwa ni  asilimia 3.8 .

Huku pia tafiti hiyo ikionyesha jumla ya watu 1,538,382 wamebainika kuishi na VVU hapa nchini,huku  ikitajwa Vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24 ni asilimia 10.6 na watoto waliochini ya miaka 15 ni 11.8 ya watu wanaoishi na VVuU nchini.
Hata hivyo,Tafiti zinaonyesha kuwa kati ya idadi hiyo wanaoishi na virusi vya ukimwi asilimia 50 ndio wanapata dawa za kupunguza makali ya VVU .

Akisoma Taarifa hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira  na watu wenye Ulemavu)Jestina Mhagama amesema licha ya ukimwa kutajwa bado ni janga hapa nchini na Duniani kutoke tafiti zinaonyesha maambukizo mpaya ya ukimwi yanadiriwa kufikia 48,000 kwa mwaka.

“Ukimwi bado ni Janga kubwa duniani na hapa nchini,Dunia imejiwekea lengo la kutokomeza Ukimwa kama janga ifikapo 2030,ili kufikia lengo hilo,yapo mashirika duniani yamejiwekea yakushirikiana na nchi mbali mbali kutokomeza ugonjwa huo”amesema Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama amesema kwa sasa serikali nchi imeendelea kufanya jitihada mbali mbali za kuhakikisha jamii inaondokana na ugonjwa huo kwa kuwahimiza wananchi kuendelea kupima afya zao ili wajitambue na kujua namna ya kujilinda.
“Licha ya kuwahimiza watu wajitokeza kupima afya zao,pia serikali inatoa wito kwa wale ambao watakutwa na maambukizo ya VVU,waanzishiwe huduma ya dawa  za kufubaza virusi vya UKIMWI, mara moja ili waweze kuishi maisha marefu na yaliyojaa na afya bora’ameongeza kusema Waziri Mhagama.
Hata hivyo,Waziri Mhagama amesema kwa sasa serikali imeanzisha mfuko wa ukimwi ambapo umepitishwa na bunge kwa sheria namba 6 ya mwaka 20015 kwa lengo la kuhakikisha uwepo wa rasimali za kutosha katika kupambana na ugonjwa huo hapa nchini.
Kwa upande wake Dr,Angella Ramandani ambaye ni Meneja mipango wa (National Aids Contoll Program)amesema kwa sasa serikali imefanya jitihada mbali mbali za kuhakikisha dawa za kufubaza za birusi vya ukimwi zinapatikana kwa wakati ili wanaondulika na ugonjwa huo iwasaidie.
“Napenda niwatoe hofu wanaogundulika na ugonjwa  wa ukimwa,jamani dawa zipo mahospitali,nawakikishia  wananchi dawa zipo,na bule kabisa”amefafanua Dr Angella.