Zinazobamba

NAIBU WAZIRI JAFFO AWAFUNDA WATUMISHI WA MANISPAA YA ILALA,SOMA HAPO KUJUA

jafo-new-4
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Utumishi na Utawala bora ,Seleman Jafo amewataka watumishi Halimashauri ya Manispaa ya Ilala kutimiza majukumu yao kikamilifu ili kuchochea maendeleo.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Anatoglo alipokuwa anazungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo wakiwemo madiwani, wakuu wa idara, Waziri Jafo ameeleza kuwa endapo kila mtumishi akitimiza wajibu wake kwa kufanya kazi kwa bidii kero na matatizo yanayowakabili wananchi yatabaki kuwa historia.

Waziri Jafo amewataka Wakurugenzi wa Halimashauri na Wakuu wa Idara kuweka mipango ya uendeshaji wa masuala mbalimbali ya kimaendeleo na kujipima wamefanikiwa kiasi gani na kama walifeli wafanyaje ili makosa hayo yasiweze kujitokeza tena, huku akiwataka kuwa wabunifu na kutafuta mapato nje ya bajeti ili waweze kujiendesha ipasavyo na kuleta maendeleo katika taifa na kuwahakikishia madiwani kushughulikiwa kuhusu suala la posho na malipo kwa watumishi.
Kwa upande wake Meya wa Halmashauri hiyo Charles Kuyeko amepongeza jitihada zinazofanywa na Naibu Waziri huyo na kumuahaidi wataendelea kuyafanyia kazi maagizo yake, ambapo akiyataja baadhi ya maagizo ambayo wameyafanyia kazi Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Palela Nitu ameeleza kuwa tayari wameunda Bodi mpya ya Soko la Samako Feri kufuatia maagizo yake, na  maboresho ya sehemu ya kuwahudumia wagonjwa wa kifua kikuu TB kwenye Zahanati ya Buyuni iliyopo Chanika.
Vilevile Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Sipora J. Liana amemueleza Naibu Waziri Jafo katika kuhakikisha jiji linaendelea, tayari wametekelezaji uboreshaji wa huduma ya usafiri kwa umma ili kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo,sambamba na uboreshaji wa huduma ya afya na mazingira.