Zinazobamba

WAZIRI MAHIGA AISIFU UN,SOMA HAPO KUJUA


http://www.tbc.go.tz/image.php?path=news_images/3844mahiga.jpg&width=600
Pichani ni Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikikiano wa Afrika Masharikia,Balozi  Dkt Augustine Mahiga


NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa Mambo ya nje na Ushirikikiano wa Afrika Masharikia,Balozi  Dkt Augustine Mahiga amesema Tanzania imepata mafanikio makubwa na uhusiano na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) katika kufanikisha  kudumisha amani na kuwaletea maendeleo wananchi .

Balozi  Dkt Mahiga ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea siku ya umoja wa Taifa  Duniani ambayo inasherekewa kila mwaka octoba 24 na mwaka huu Shirika hilo linatimiza miaka 71 tangu kuanzishwa kwake.

Amesema Tangu Tanzania kujiunga uwanachama na Shirika hilo limepata mafanikio makubwa ikiwemo kuletewa maendeleo mbali mbali inayotokana na misaada inayotolewa na shirika hilo pamoja na kudumisha amani.

Amedai kuwa shirika hilo linasimamia na kuhakikisha nchi zote ziliko nchini ya umoja wa Mataifa yanahakikisha yanadumisha amani jambo analodai linastahiri kupongezwa kwa shirika hilo.
Ameongeza kuwa kwa sasa serikali itahakikisha inadumisha uhusiano na shirika hilo kwani wamebaini linamchango mkubwa katika kuwaletea maendeleo wananchi wake pamoja na kudumisha uhusiano na mataifa makubwa.
Amekumbusha kuwa UN imeleta mchango mkubwa wakati wa kufanikisha nchi kupata uhurukwa kudai kuwa  shirika hilo lilikuwa linatoa nguvu kwa Taifa kuhakikisha  tunajikomboa na kupata uhuru,
Kwa Upande wake Kaimu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini,Bi Chansa Kapaya amesema kwa sasa Tanzania na umoja wa mataifa zimekuwa na ushirikiano kwa miaka mingi,
Amesema ni wakati kubadilika kwa Tanzania kutokana na misaada mbali mbali inayotolewa na umoja  mataifa  huku akitaka kukidhi haja mpya husasani kwa kipindi cha Taifa linapoelekea uchumi wa kati.