Zinazobamba

SAMIA SULUHU AMSHAMBULIA KIKWETE WAZI WAZI,SOMA HAPO KUJUA



Dk. Jakaya Kikwete, Rais mstaafu wa Tanzania
SAMIA Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ‘ameikandia’ Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete na kusema imeacha mzigo mkubwa wa madeni, anaandika Dany Tibason.
 
Samia amesema kutokana na mzigo mkubwa wa madeni ambao wameirithi kutoka katika serikali ya awamu ya nne, licha ya serikali kukusanya Sh. 1.3 trilioni kwa mwezi lakini madeni yanayolipwa kila mwezi ni Shilingi bilioni 900.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akifungua mkutano wa waganga wakuu wa mikoa, halmashauri na waganga wafawidhi wa hospitali za mikoa na kanda mbalimbali hapa nchini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.

“Huu siyo wakati wa kutegemea kila kitu kutoka serikalini, kusema ukweli kwa bahati mbaya tulipoingia madarakani tulikuta madeni makubwa ambayo yaliachwa na serikali ya awamu ya nne, lazima tulipe madeni hayo,” amesema.
Bila kutoa ufafanuzi wa madeni hayo kama ni ya ndani au nje ya nchi Mama Samia amesema serikali ya awamu ya tano ilikutana na mzigo mkubwa wa madeni ambao haukwepeki kwani serikali inapoingia madarakani hurithi madeni na mali za serikali iliyomaliza muda wake.
Amezitaka hospitali za serikali kote nchini kuepuka migogoro katika sekta ya afya kwa kufunga mitambo ya kielekroniki kwa ajili ya kukusanya mapato ambayo yatawezesha ulipiaji wa mahitaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na ununuzi wa madawa.
“Serikali bado inajipanga kuona ni jinsi gani ya kuwezesha katika sekta muhimu na ndiyo maana serikali ya awamu ya tano imeweza kupitisha bajeti kubwa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto tofauti na miaka yote tangu nchi ipate Uhuru,” amesema Samia.