MANISPAA YA ILALA YAFAFANUA KUHUSU TAARIFA YA UKATILI KWA WATOTO,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
MANISPAA ya Ilala imesema katika kipindi cha mwezi
Januari hadi Agost mwaka huu jumla ya watoto 302 wameripotiwa kufanyiwa ukatili wa kingono.
Ambapo kati yao, watoto 130 ni wakike ambapo ni sawa na
asilimia 43% wameripotiwa kubakawa,huku watoto wakiume 24 sawa na asilimia 7.9%
wameripotiwa kufanyiwa vitendo vya kulawitiwa.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Afisa
Uhusiano wa Manispaa hiyo,Tabu Shaibu wakati wa mkutano na waandishi wa habari
ili kutoa ufafanuzi juu ya manispaa ya ilala kutajwa kuwa kinara kwa vitendo
vya ubakaji.
Amesema kamati
ya ulinzi na usalama wa mtoto imefanya utafiti kupitia madawati mbali
mbali ya kijinsia yaliyopo kwenye vituo vya Polisi katika manispaa hiyo
wamebaini kuwepo kwa matukio hayo ya kinyama kwa watoto.
“Katika Tathimini ya awali iliofanywa imeonyesha
kuwepo kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto hususani matukio ya
ukatili wa kingono(watoto kubakwa na kulawitiwa) majumbani kwa watoto chini ya miaka 18”amesema Afisa
Shaibu.
Amesema Sababu waliyoibaini kupelekea kwa vitendo
hivyo katika manispaahiyo imechangiwa na uwezo mdogo wa kujitetea kwa watoto
hao jambo linalopelekea kufanyiwa vitendo hivyo,
Afisa huyo pia ametolea ufafanuzi ulioripotiwa na
Vyombo vya habari kuwa kati ya watoto 10 katika manispaa ya ilala watoto 7
wamefanyiwa ukatili wa kingono,huku akidai ripoti hiyo haikuwa sahihi.
Pamoja na hayo,Afisa Shaibu ametoa hofu wazazi na
walezi wa watoto katika manispaa hiyo kuondoa hofu waliokuwa nayo kutokana na
taarifa hiyo kwa watoto,