Zinazobamba

WAFANYABIASHARA WA MWENGE WAGOMEA UKUTA YA CHADEMA,SOMA HAPO KUJUA




WAKATI ikiwa imebakia siku moja ili Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutekeleza hadha yao ya kufanya maandamano na mikutano ya hadhara nchini kwa kile wanachosema kupinga Udikteta nchini.

Nao wafanyabiashara wadogowado wa soko la stendi ya Mwenge Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam wamesema hawatashirikia maandamano hayo.


Wamesema maandamano hayo hayana tija kwa sasa,yanalengo ya kuwagawa watanzania.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao ,Omary Hamis amewaambia waandishi wa habari leo Jijini Hapa wanaungana na Rais John Magufuli katika kile anachokiita ni harakati za Rais huyo kumkomboa mtanzania myonge,

Amesema anawambomba vijana wasikubali kurubuniwa  na wanasiasa huku akiwataka kujikita katika kufanya kazi kwa bidii na kuachana na maandamano hayo.