Zinazobamba

FREEMAN MBOWE AMEJAA BUSARA,HATUA YA KUSITISHA UKUTA,WANANCHI WAMFAGILIA KILA KONA NA WAMUONYA JPM,SOMA HAPO KUJUA




Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ametangaza kusitishwa kwa maandamano ya Oparesheni UKUTA yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kesho nchi nzima.

Mbowe ametoa kauli hiyo ya kuahirisha maandamano mchana huu wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari.

Amesema sababu kubwa za kuahirisha maandamano hayo ni busara zaviongozi wa dini ambao wameiomba Chadema iwape muda wa   kutafuta Suluhu 

Mbowe amesema maandamano hayo yameahirishwa hadi Oktoba Mosi ili suluhu ipatikane kwa viongozi wa dini watakapokwenda kukutana na Rais John Magufuli
  WANANCHI WAMPONGEZA MBOWE.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi mbali mbali wampongeza Mwenyekiti huyo ambaye ni mbunge wa Jimbo la Hai wamesema hatua ya kuzuia maandamano ni jambo jema huku wakisema  mwenyekiti huyo ni mtu makini na ni mlezi wa amani ya Tanzania.

Ally Salum Ally mkazi wa Magomeni amesema licha ya viongozi wa serikali ya awamu ya tano kusinya katiba ya Jamhuri wa Muungano lakini bado vyama vya siasa kikiwemo chadema kuonyesha utulivu wa kisiasa.

Amefafanua kuwa hatua ya serikali kuminya katiba jambo hilo lingetokea katika nchi zengine basi amani ya Tanzania ingekuwa rehani.

Hata hivyo Ally amemuomba Rais John Magufuli kuwasilikiza kwa makini viongozi wa dini pindi wakimtembelea na akubali kutafuta suluhu la vyama vya siasa kwani bila siasa makini basi serikali ya viwanda anayoitaka, ataishia kuiimba jukwaani.
"Huyu mbowe ni mtu makini sana na amewasilikiza viongozi wa dini,kwani mtu mwenye maono uwasikiliza viongozi wa kiroho,na mbowe ameonyesha umakini wake,hata sisi tunamuomba Mungu ampe nguvu mbowe aendelea kuwa na uvumilivu kama huu.na tunamuomba Rais Magufuli naye aige mfano wa Mbowe"amesema Joseph Kesi mkazi wa Morogoro