Zinazobamba

VIJANA WAPEWA NENO KUHUSU UKOSEFU WA AJIRA,SOMA HAPO KUJUA

Pichani ni Naibu Waziri,Ofisi Waziri Mkuu,Sera,vijana na watu walemavu,Abdalla Posi



VIJANA wametakiwa kubuni mipango ya kijiajiri pinda wanapokuwa shuleni ili waweze kuondokana na dhana ya kujiajiri pindi wanapomaliza shule.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo

Wito  huo umetolewa Leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri,Ofisi Waziri Mkuu,Sera,vijana na watu walemavu,Abdalla Posi wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Great Hope ambayo ni taasisi ya  kuwawezesha wanafunzi fursa ya kuvionyesha vipaji vyao pindi wanapokuwa shule ili waweze kujiari pindi watakapomaliza shule.

Ambapo Possa amesema kwa sasa Taifa limekuwa likikabiliwa na
changamoto ya vijana kutegemea kujiajiri jambo analodai limechangiwa na vijana wenyewe kuwa waoga wakutuhubutu kujiajiri.

Amesema endapo vijana wakionyesha njia ya kujiwekea mipango mizuri ya baadae pindi wanapokuwa shuleni itaweza kuwaisadia kufanikiwa pindi watakapomaliza shule katika kupanga mipango mizuri ya ajira kuacha kuwa tegemezi.

Hata Hivyo,Posa ameipongeza taasisi hiyo kuanzisha mpango huo ambao anadai utaweza kuwasaidia vijana katika kujikwamua kimaisha.

Kwa Upande wake Mratibu wa Taasisi ya Great Hope,Noelle Mahuvi amesemania iliyomugusa kunzisha ni baada ya kushuhudia mazingira magumu ya wanafunzi pindi wanapomaliza shule baada ya kukosa ajira.
Amesema mpango aliounzisha utaanza katika shule kadhaa jijini dar es
Salaam kwa lengo la kutekeleza mpango huo.