SHOGA AIPONZA CLOUDS TV,TCRA YAKUNJUA MAKUCHA YAKE NA KUIPIGA PINI,SOMA HAPO KUJUA
Ruge Mutahaba, Mkurugenzi wa Clouds Media Group |
MAMLAKA ya mawasiliano nchini (TCRA)
imetoa onyo pamoja na kuutaka uongozi wa Clouds TV kuomba radhi Watanzania
kupitia taarifa zake za habari ndani ya siku tano mfululizo kuanzia leo,anaadika Regina Mkonde.
Adhabu hiyo imetolewa leo na kamati ya Maudhui ya TCRA,
baada ya baadhi ya wananchi hususani watazamaji wa kipindi cha ‘Take One’
kilichorushwa 28 Juni mwaka huu ambacho kilidaiwa kueleza masuala ya mapenzi ya
jinsia moja (Ushoga), kulalamikiwa kwamba kilikiuka maadili ya taifa.
Wakati akisoma
tamko la adhabu hiyo, Joseph Mapunda, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo amesema
kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya wajumbe wa kamati kutafakari maelezo ya
utetezi yaliyotolewa na uongozi waClouds TV.
“Tumetafakari
kwa kina maelezo ya utetezi yaliyotolewa na clouds tv kuhusu kipindi chake cha
Take One kilichorushwa hewani tarehe 28 June 2016 ambacho kilikiuka baadhi ya
kanuni za maadili ya utangazaji,” amesema Mapunda.
Ameongeza kuwa
“kutokana na kipindi hicho kuwakwaza pamoja na kuwasababishia usumbufu wananchi
hususan watazamaji kwa kuwasilisha mada inayozungumzia masuala ya mapenzi ya
jinsia moja (ushoga), Clouds TV inatakiwa kuwaomba radhi watanzania wote na
watazamaji.”
Amesema taarifa
ya kuomba radhi itoke siku tano mfululizo katika taarifa zao za habari ya saa
moja na nusu na ya saa tano usiku kuanzia siku ya kusomwa hukumu, na kwamba
uthibitisho wa taarifa hizo upelekwe TCRA siku ya Jumatano tarehe 13 Julai 2016
kabla ya saa kumi jioni.
“ Hatua ya pili,
Clouds Tv inatakiwa kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza na kuhakikisha
inazingatia kanuni zote za utangazaji nchini katika kutekeleza majukumu yake ya
utangazaji,” amesema na kuongeza.
“Kamati
inawaonya vikali Clouds tv kwa kukiuka kanuni za huduma za utangazaji (maudhui)
ya mwaka 2005, namba 5(b), 5(c), 5(d) na 15(c) 16(2) uamuzi huu umetolewa leo,
haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu iko wazi ndani ya siku 30 tangu siku
uamuzi unapotolewa.
Ruge Mutahaba,
Mkurugenzi wa Clouds Media Group amesema baada ya kutafakari tamko la adhabu
atatoa msimamo wake kama wataka rufaa au la.
“Tunaweza
tukarudi nyuma na kusema tufanye kazi ya kukata rufaa, kwa sababu tunaamini na
mimi nina simamia msimamo wangu kwamba tunapoambiwa tunalinda maadili ya
kitaifa, kupinga jambo lolote baya ni kulinda maadili ya kitaifa,” amesema na
kuongeza.
“Sasa ukiambiwa
kwamba ulipinga kwa namna ya ulivyo pinga ni tofauti kidogo labda inaweza
ikasaida kutengeneza mjadala mkubwa wa kujiuliza maadili tunayotakiwa kuyalinda
ni yapi.”
Mutahaba amesema
“Lakini moja kati ya kitu tunachokiona kina utofauti ni kuna baadhi ya mambo
yamezungumzwa ambayo sikumbuki kabisa kama yako kwenye kipindi, kwa hiyo sijui
wamezitolea wapi.”
Amesema kuwa
ushoga ni tatizo na kwamba lazima alikemee na ataendelea kulikemea.
“Kwa ajili ya
kosa la kutaja neno shoga katika kipindi cha njia panda mwaka 2000, miaka minne
iliyopita kwenye gazeti tulivyosoma neno ushoga tukatozwa faini ya mil 5,
haiwezekani miaka kumi na sita inapita kutaja neno shoga kila siku mtu anapewa
adhabu,” amesema
Hakuna maoni
Chapisha Maoni