Zinazobamba

TRA YAHIMIZA WANANCHI KUTOA KODI,YATOA DARASA TOSHA CHUO CHA IFM,SOM HAPO KUJUA



NA KAROLI VINSENT
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imesema maendeleo mazuri watanzania  wanayoshudia katika nchi zilizoendelea yametokana na wananchi  katika nchi hizo kuwa na bidii  katika kutoa kodi,

Hivyo,Mamlaka hiyo imewasihi watanzania kuwa wazalendo na kutoa kodi kwa bidii  ili waweze kuliunua Taifa kimaendeleo.

Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa (TRA) Richard  Kayombo wakati wa ufunguzi wa Klabu ya  Wanafunzi mamlaka  hiyo katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)

Kayombo amesema kwa sasa Taifa la Tanzania ili litoke hapa lililo linaitajiaka juhudi kubwa kwa watanzania kutoa kodi kwa bidii ili serikali iweze kutumia kodi hiyo katika kuleta maendeleo mbali mbali.

Amesema Kodi ndio njia ya msingi ambayo itaweze kuondoa malalamiko yanatolewa kutoka kwa wananchi ikiwemo kukosa huduma muhimu kama hospitali pamoja na barabara.
Kayombo ametolea mfano hata ujenzi wa Barabara ya mabasi yaendeyo kasi yametokana na serikali kukopa fedha kwenye taasisi ya kimataifa kwa kutugemea kurejesha fedha hizo kwa mapato yatakanayo na makusanyo ya kodi.
 
Hata Hivyo,Kayombo amewataka wanafunzi  wa IFM kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza jamii wanazotoka katika kuhimiza kutoa kodi ili maendeleo ya serikali yafikiwe kwa wakati.

Kwa Upande wake Makamu mkuu wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha IFM,Felician Mussa ameishukuru Mamlaka hiyo kwa hatua waliyofanya katika kufungua Klabu hizo Chuoni  hapo huku akisema wanafunzi wenzake watakuwa Mabalozi wazuri katika kuhimiza jamii katika ukusanyaji wa kodi.





Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) katika ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi Vyuoni jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa jumuiya wa wanafunzi wa Kodi katika chuo cha usimamizi wa fedha (IFM), Amos Ojode akizungumza na kuwashukuru wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo cho kujifunza na kuzindua jumuiya ya wafunzi wa kaodi vyuoni katika chuo chao.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wakiwa katika uzinduzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi katika chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) jijin Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo  akizungumza na wanafuzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi vyuoni.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) wakiwa katika uzinduzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi katika chuo chao jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Elimu kwa Mlipakodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana masala akizungumza na wanafuzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi vyuoni.
 Waziri wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) akizungumza na kuwashukuru wafanyakazi wa TRA kwa kuzindua Jumuiya ya wanafunzi wa kodi jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa  chuo cha usimamizi wa fedha (IFM), Elius Mbogo akizungumza na kuwashukuru wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo cho kujifunza na kuzindua jumuiya ya wafunzi wa kaodi vyuoni katika chuo chao.


Hakuna maoni