SHEIKH PONDA TENA,SAKATA LAKE KUFUKILIWA UPYAA,SOMA HAPO KUJUA
SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislam nchini, bado anawindwa na mawakili wa serikali, anaandika Faki Sosi.
Mawakili hao wanapinga hukumu
yake iliyotolewa na Richard Kabate, Hakimu Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro mwaka
jana ya kumfutia makosa ikiwemo la uchochezi.
Jana
katika Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Jaji, Edson
Mkasimongwa, Bernard Kongola ambaye ni Wakili Mkuu Mwandamizi wa Serikali
amesema kuwa, Jamhuri inapinga hukumu hiyo.
Mwaka
2013 Sheikh Ponda alishitakiwa kwa makosa matatu; la kwanza alidaiwa kuwaambia
waumini wa Dini ya Kiislam kwamba, wasikubaliane na uundwaji wa kamati za ulinzi
na usalama za misikiti zilizoanzishwa na Baraza Kuu la Waislam Tanzania kwa
madai ni vibaraka wa CCM na serikali.
Shitaka
la pili lilihusu kuwa, Sheikh Ponda aliwaambia Waislamu kwamba serikali
ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi ili
kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi hao ni
Waislamu.
Shitaka
la tatu alidaiwa kulitendwa tarehe 10 Agosti mwaka 2013 kuwa, kauli yake katika
shitaka la pili inadaiwa kuumiza imani za watu wengine kinyume cha kifungu cha
sheria namba 390 na kanuni ya adhabu namba 35 cha mwaka 2002.
Wakili
Kongola amesema, uamuzi uliotolewa na Hakimu Kabate haukuzingatia uzito wa
ushahidi wa Kielekroniki uliofikishwa mbele ya mahakama yake.
Wakili
Kongola amesema kuwa, hakimu alikosea aliposema kuwa hati ya mashitakaa ina
upungufu kisheria na kuwa Shekh Ponda hakuwa na nia ya kuwashawishi
waumini kufanya kosa.
Amesema
kuwa, hakimu alikosea pale aliposema upande wa mashitka
haukuthibitisha mashitaka mahakamani. Rufaa hiyo imepangwa kuanza
kusilizwa rasmi tarehe 30 Juni mwaka huu.
Mwishoni
mwa Novemba mwaka jana, Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro ilimuachia huru
Sheikh Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama
hiyo kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka.
Awali
Bernard Kongola, Mwanasheria Kiongozi wa Serikali mbele ya Richard
Kabate, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro alidai kuwa, tarehe10
Agosti mwaka 2013, katika eneo la Uwanja wa Ndege, Manispaa ya Morogoro, Sheikh
Ponda alifanya uchochezi jambo lililosababisha kufunguliwa mashitaka hayo
matatu.
Na
kwamba, awali katika agizo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyotolewa na
Hakimu Victoria Nongwa tarehe 9 Mei mwaka 2010, Sheikh Ponda ndani ya mwaka
mzima alitakiwa kuhubiri amani na kuwa raia mwema jambo ambalo alishindwa
kulitekeleza.
Katika
kesi yake Sheikh Ponda alikuwa akitetewa na wakili wake Juma Nassor
Hakuna maoni
Chapisha Maoni