Zinazobamba

UKAWA WAPAMBANA NA MAJANGILI WA TEMBO BUNGENI,WASHIKA PABAYA SERIKALI YA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA


Tembo aliyeuwawa na majangili
Tembo aliyeuwawa na majangili




OPERESHENI Tokomeza Ujangili iliyofanyika tarehe 4 Oktoba 2013 haijafika kikomo. Vyama Vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) leo bungeni vimedai idadi ya majangili waliokamatwa, anaandika Faki Sosi.

Ni kwa kuwa, mpaka sasa wameeleza kutoona matokeo ama utekelezwaji wa maazimio ya bunge yaliyofikiwa kutokana na operesheni hiyo.

Ni operesheni ilisababisha Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa mawaziri wake wanne kufuatia wabunge kuungana bila kujali itikadi za vyama vyao kupinga unyanyasaji uliofanywa wakati huo.
Mawaziri walioondolewa walikuwa David Mathayo (Mifugo), Dk. Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii) ambaye alijiuzulu.

Esther Matiko, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni katika Wizara ya Maliasili na Utalii wakati akiwasilisha maoni ya upinzani kuhusu Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 leo amesema;
“Ni muda mwafaka sasa Kambi Rasmi kutaka kuelewa ni majangili wangapi baada ya operesheni hiyo kumalizika mali zao zimekamatwa na tayari kesi zao ziko mahakamani au tayari wamefungwa?”
Esther amesema, pamoja na operesheni hiyo kuwa na athari kubwa lakini watu wengi walioathirika hawajalipwa fidia zao mpaka sasa.
Mefafanua kuwa, kwa mujibu wa Taarifa ya Serikali, vitendo vya ujangili vinavyofanyika nchini vimegawanyika katika makundi mawili
Kundi la kwanza ni Ujangili wa Kujikimu; na kwamba aina hii inahusisha watu wenye kipato kidogo na hulenga zaidi katika kujipatia kitoweo na fedha kwa ajili ya kukidhi mahitaji mengine.
Aina ya pili ni Ujangili wa Biashara; Aina hii ya ujangili inahusisha zaidi watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha na hulenga kupata nyara zenye thamani kubwa.
“Wanyama wanaoathiriwa zaidi na aina hii ya ujangili ni pamoja na Tembo, Faru, Simba na Chui,” amesema.
Amesema “…tarehe 04 Oktoba 2013 ilizindua Operation Maalum ya kupambana na ujangili huo ili kuzuia vitendo hivyo ndani na nje ya hifadhi za Taifa, katika Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu.
“Pia kuwatambua mapema majangili na kujua nyendo zao ndani na nje ya maeneo ya hifadhi kwa kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wahusika wakuu wa nyara hizo za Taifa.”
Amesema, Rais Jakaya Kikwete aliunda tume maalum iliyoongozwa na Mhe Jaji Msumi ya kushughulikia suala hilo, lakini taarifa ya tume hiyo hadi sasa imeishia kwenye makabati ya Ikulu na Watanzania hawakupata nafsi ya kuelewa nini Jaji Msumi aliona na kushauri.
“Aidha hakuna hatua zozote za fidia zimechukuliwa kwa waathirika wa operation hiyo ambao wengi walipoteza mifugo yao, walichomewa nyumba zao, walibakwa, walidhalilishwa na wengine walipoteza ndugu na jamaa zao na wengine wamekuwa walemavu.

Hakuna maoni