Zinazobamba

SERIKALI YATANGAZA AJIRA 71,496,SOMA HAPO KUJUA


SERIKALI itaajiri watumishi wa kada mbalimbali 71,496 mwaka wa fedha 2016/17.Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mbulu Mjini (CCM), Zacharia Issaay.

Mbunge huyo alihoji kuwa nafasi za watendaji wa vijiji na kata zimekuwa wazi ni kwanini serikali isione umuhimu wa kutoa nafasi kwa vijana waliomaliza vyuo kuanza kujitolea katika kipindi cha mpito ili baadae waingie kwenye mfumo wa ajira.
  
Kairuki alisema pamoja na ufinyu wa bajeti, serikali katika mwaka ujao wa fedha unaoanza Julai, mwaka huu, itaajiri watumishi wa kada mbalimbali, wakiwamo watendaji wa vijiji na kata ambapo ajira zao zitaanza kutolewa mwezi huu. 
  
“Serikali imekuwa ikipandisha kima cha chini cha mshahara kulingana na uwezo wa bajeti (mapato ya ndani) na kwa kuzingatia gharama za maisha,” alisema.
  
Kairuki alisema maombi ya nafasi za ajira serikalini hufanyika kwa uwazi kupitia bajeti ya serikali ambayo huidhinishwa na Bunge.
  
Alisema nafasi hizo za ajira hutolewa baada ya waajiri kuwasilisha maombi yao serikalini na kuidhinishwa kwa kuzingatia ukomo wa bajeti ya mishahara serikalini.
  
Aidha, Kairuki alisema Tanzania ni moja ya nchi za Afrika ambazo hulipa kima cha chini cha mshahara sawa na asilimia 80 ya kiwango cha gharama za maisha.

Hakuna maoni