WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI KUJA NA HIKI,SOMA HAPA KUJUA
Mbunge wa
Bunge la Afrika Mashari Makongoro Nyerere akizungumza na waandishi wa
habari(Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na wabunge wa bunge la
Afrika Mashariki kuanza kuhamasisha jamii kuchangamkia fursa za kibiashara
zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kutoka kulia kwenda kushoto ni
Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Banji, Miriam Yahaya Usi,
Ndarakilo Kessy na Dk.Twaha Tasilima wakiwa katika mkutano huo leo.
|
WABUNGE wa Jumuiya la Afrika Mashariki kuanza
kuhamasisha jamii ili kujua fursa za Kibiashara zilizopo katika Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Ameyasema hayo leo Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa wataanza kuhamasisha jamii katika soko la Kariakoo na Soko la Samaki la Feri jijini Dar es Salaam pamoja na vyombo vya habari mbalimbali.
Makongo amesema kusudi la kuelimisha jamii ili wafanyabishara waweze kufanya biashara katika nchi za Afrika Mashari kama Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi
Amesema kuwa frusa zilizopo kwa waalimu wa Lugha ya Kiswahili wanaweza kwenda kufundisha Kiswahili kwenye Nchi za Afrika Mashariki ikiwa ni Kenya Uganda, Rwanda, Burundi na Afrika ya kati ipo mbioni kujiunga na Umoja huo.
Amesema Lugha ya Kiswahili kwa sasa imeanza kushika karibu nchi zote za Afrika Mashariki na hii ndio fursa Kubwa tuliyo nayo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni