Zinazobamba

MTEULE WA MAGUFULI APOPOLEWA,SOMA HAPO KUJUA



 John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza


JOHN Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amemvaa Justus Kamugisha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza kwamba alikuwa mzigo, anaandika Moses Mseti.

Amesema, Kamanda Kamugisha ndiye aliyesababisha kuwepo kwa matukio ya uhalifu mkoani humo na kisha kushamiri.

Mongella amedai kuwa kuhamishwa kwake kutoka mkoani humo kutasaidia kupunguza vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha za moto uliokuwa ukifanyika kila baada ya siku mbili na kujenga hofu.

Kamugisha ambaye amehamishiwa mkoani Mbeya, alipokuwa kamanda wa polisi mkoani Mwanza, matukio zaidi ya saba ya uhalifu wa kutimia silaha za moto yalitokea ndani ya kipindi cha miezi mitatua.

Mongella alitoa kauli hiyo jana katika mkutano na watumishi wa Halmashauli ya Wilaya ya Magu ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha kwa watumishi na viongozi mbalimbali wa mkoa huo.
“Huyu kamanda wetu (Justus Kamugisha) ndani ya wiki mbili tangu anaingia Mwanza, matukio ya uhalifu wa kutumia silaha yalizidi kuongezeka, ni bora umehamishiwa Mbeya labda huko ni kwepesi,” amesema Mongella.
Mongella amesema kuwa, Mkoa wa Mwanza hususan jijini Mwanza, matukio ya uhalifu yalikuwa tishio kutokana na kutokea mara kwa mara.
Hata hivyo, Mongella amesema kuwa hatasita kuwachukulia hatua za kinidhamu na kisheria Wakuu wa Polisi Wilaya watakaoshindwa kudhibiti vitendo vya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.

Hakuna maoni