Zinazobamba

BARAZA LA MAWAZIRI LA MAGUFULI LAANZA KUCHAFUKA,WAZIRI WAKE AHUSISHWA KWENYE KASHFA YA BILIONI 37 NDANI YA JESHI LA POLISI,SOMA HAPO KUJUA

Pichani ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ambaye ameingia kwenye Kashfa ndani jeshi la Polisi


Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34, imeelezwa.
Kuhusika huko kwa Waziri Kitwanga imekuja siku moja, baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) kueleza kuwa kuna ufisadi mkubwa kwenye mkataba ulioingia kati ya Jeshi la Polisi Nchini na Kampuni ya Lugumi Enterprises.
Taarifa za kuaminika ilizozipata gazeti hili, zimeeleza kuwa Waziri Kitwanga anahusika kupitia kampuni yake ya Infosys anayomiliki pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), iliyo chini ya Wizara hiyo hiyo.
Jeshi la Polisi limekumbwa na kashfa kubwa ya manunuzi ya vifaa vya kuhifadhi alama za vidole ambapo Kamati ya PAC imegundua kuwa kampuni ya Lugumi Enterprises haikutekeleza mkataba ipasavyo.
Kampuni hiyo ililipwa sh. bilioni 34 na jeshi la polisi ili kusambaza vifaa hivyo nchi nzima katika vituo 138 vya polisi lakini ni vituo 14 vilivyopata vifaa hivyo.
Gazeti hili limegundua kuwa moja ya kampuni iliyopewa kazi hiyo ni Infsosys ambayo nakala za msajili wa makampuni inaonyesha kuwa inamilikiwa na Charles Kitwanga na Dk. Modestus Francis Kipilimba, ambaye ni Mkurugenzi wa NIDA.
Nyaraka za uchunguzi ikiwemo mkataba kati ya kampuni ya Lugumi na Infosys ambazo gazeti hili imeziona inaonyesha kuwa Kampuni hiyo ya Waziri Kitwanga ilifanya kazi ya kuunganisha internet kati ya vituo vya polisi na mkonga wa taifa.
Kazi ambayo haikufanyika kabisa kwani mpaka sasa ni vituo 14 tu vya polisi viliunganishwa, ambapo baadhi ya taarifa ilizozipata gazeti hili zilionyesha kuwa moja ya taarifa ya ukaguzi inaonekana Marijani Saleh alisaini kufikisha vifaa vya Infosys.
Vifaa hivyo, vinaelezwa vilifikishwa Machi 2, 2012. Katika Nyaraka hiyo upande wa Jeshi la Polisi alisaini ofisa mmoja wa Polisi aliyejulikana kwa jina la Nestory Tagaya na mdau mwingine kutoka kampuni ya BioLink alikuwa Pierson J.
Taarifa iliyotolewa na PAC hivi karibuni ilionyesha kuwa kampuni ya Lugumi ilingia mkataba na Jeshi la Polisi mwaka 2011, kwa kazi hiyo ya kufunga mitambo hiyo kwenye vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima na kulipwa fedha zote huku kazi ikiwa haijafanyika

Hakuna maoni