Zinazobamba

MOSHI KWENYE IKULU YA MAGUFULI WATAFUTIWA DAWA,MANISPAA YA ILALA YAJA NA HICHI,SOMA SOMA HAPO KUJUA


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi akitangaza matokeo ya Umeya na Unaibu Meya katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo
Pichani ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Isaya Mgurumi
NA KAROLI VINSENT.
KATIKA kuhakikisha wanakabiliana na Moshi wa samaki katiko soko la feri jijini Dar es Salaam ambao ulikuwa unaibuguzi Ikulu ya Rais John Magufuli,
Hatimaye Manispaa ya Ilala imetafuta ufumbuzi wa kadhia hiyo Mara baada ya kununua majiko 48 mapya na ya kisasa ambayo yatatumiwa na wapishi wa samaki katika soko hilo.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Isaya Mgurumi wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kwa sasa Manispaa hiyo baada ya kutambua kadhia hiyo imenunua majiko 48 mapya ya kisasa ambayo yanatumia nishati ya Gesi  kwa ajili ya kutatua tatizo hilo.
“Majiko haya 48 ya Gesi yatatumika kwa ajili ya kupikia wauza samaki katika soko la feri kwani matumizi haya ya jiko la gesi yatasaidia kuondokana na Moshi mkubwa ambao ulikuwa unatoka katika soko hilo,na moshi huo tumechunguza tumejua ulikuwa unatokana na matumizi ya mwanzo ya nisharti ya kuni,”amesema Mgulu,
Amesema hatua ya sasa iliyobakia ni kufunga Gesi kwenye majiko hayo pamoja na kuweka uzio wa Bati ili iweze kuwasaidia wauza samaki hao kujikinga na mvua zinazonyesha,
Sanjari na hilo amesema kwa sasa Manispaa hiyo imedhamilia kuweka mazingira safi katika soko hilo ili kuhakikisha wanazuia magonjwa ya mlipuka ambayo yanayoweza kutokea kutokana na uchafu katika soko hilo.
Katika hatua nyengine Manispaa hiyo imesema zoezi la umoaji wa jengo la gorofa 16 kwenye mtaa wa Indira Ganji jijini hapa unaendelea vizuri mara baada ya Manispaa hiyo kushirikiana na idara mbali mbali za serikali kumpata mkandarasi atakaye livunja jengo hilo,
Amesema mkandarasi huyo mzawa ametokana mara baada ya kampuni sita kujitosa kwenye ushindani wa tenda la kuvunja jengo hilo huku,Kampuni tano zikishindwa na tenda hiyo ambapo Kampuni ya kizawa ndio iliyoshinda tenda hiyo yenye thamani ya milioni 900.
Amefafanua kuwa katika kipindi cha siku tatu tangu kampuni hiyo ya kuanza uvunjaji huo,teyari Kampuni hiyo imevunja gorafa tatu. Huku akisema Kampuni hiyo imepewa siku 60 iwe imemaliza kazi ya kulivunja jengo hilo.

Hakuna maoni