Zinazobamba

WAZIRI MWAKYEMBE AING'ANG'ANIA KATIBA YA SITTA,AIBUKA NA KUSEMA KIPORO CHAKE LAZIMA KIMALIZIWE,SOMA HAPO KUJUA

WAZIRI wa Katiba na sheria,Dk Harrison Mwakyembe ni kama ameanza kujiingiza kwenye msuguano na wanasiasa,viongozi wa dini,mara baada kusema mchakato wa kumalizia kiporo cha Katiba mpya huko palepale.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara kwenye ofisi ya Mwendesha mastaka wa serikali nchini,DPP ambapo amesema suala la kuendelea na mchakato wa kuipigia kura katika iliyopendekezwa na iliyokuwa Bunge maalum la Katiba ipo pale pale kinachosubiliwa ni Rais John Magufuli kutangaza siku ya kura ya maoni.
“Jamani wote kwa pamoja mlimsikia Rais Magufuli amesema anakiporo cha Katiba mpya,,maana yake Rais ni mkuu wanchi ameshasema na kila mtu alimsikia kwahiyo mchakato wa kupiga kura  katiba pendekezwa upo palepale”amesema Waziri Mwakyembe.
Kauli hii ya Mwakyembe juu ya uwepo wa kuendelea na mchakato wa katiba mpya unaweza kuibua majadala mkubwa na kuleta sintofahamu,kwani kipindi kile wakati lilokuwa Bunge maalum la Katiba lilivyokuwa linatunga Katiba Pendekezwa kuliibuka msuguano mkubwa kati ya serikali na viongozi wa dini na wanasiasa.
Wote kwa pamoja wanasiasa na viongozi wa dini waliitoa matamko na kudai hawaitaiuunga mkono Katiba pendekezwa kwa madai imeshindwa kuendana na maoni ya wananchi yaliyotokana na iliyokuwa tume ya ukusanyaji maoni ya kwenye Katiba mpya,iliyongozwa  Jaji Warioba.
Katika hatua Nyengine Waziri Mwakyembe ametoa masikitiko yake kwa kudai wizara ambazo anaziona zitamwangusha Rais Magufuli ni wizara ya Katiba na sheria ambayo inayoiongoza pamoja na Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi inayoongozwa na Waziri Chalres Kitwanga kwa madai ndizo zinakithili kwa rushwa.
“Hizi wizara kusema kweli zinanuka rushwa azitendi haki zimekuwa zinawabambikia watu kesi kwa makusudi kwa kisingizio cha kutaka pesa,na wakiendelea hivi lazima kasi ya Rais Magufuli itapunguzwa na watu hawa”amesema Mwakyembe.
Waziri Mwakyembe amebainisha kuwa hata kubali kuona kasi ya Rais Magufuli inaangusha na watu wa wizara yake kwani amedai kuwafukuza kazi watumishi ambao atawabaini wanapokea rushwa.

Hakuna maoni