Zinazobamba

SERIKALI YA MAGUFULI KUYAFUNGIA MAGAZETI HAYA,NI YALE YALIOKUWA YANAMSAKAMA LOWASSA NA MBOWE,SOMA HAPO KUJUA


Pichani ni mkurugenzi wa Idara ya Habari maelezo,Assah Mwambene

GAZETI la Jambo leo na Raia Tanzania yote  kwa pamoja ambayo yanatoka kwa siku, yako mbioni kufungiwa na Serikali ya Rais John magufuli.(Mtandao huu umedokezwa).Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Ofisi ya msajili wa Magazeti  nchini,ambazo mtandao huu umezipata zinasema kwa sasa  ofisi hiyo ya msajili itafikia uamuzi baada ya  kubainika Magazeti hayo yamekiuka sheria ya magazeti ya mwaka 1976.
Makosa ambayo yanadaiwa kufanywa magazeti hayo ni ile ya wamiliki wa magazeti hayo kuyauza kinyemela bila ya hata kuishirikisha ofisi ya msajili wa magazeti nchini kama sheria ya magazeti inavyokata,pia kuchangia kuikosesha serikali mapato kutokana na uuzwaji huo .
Taarifa za magazeti hayo kuuzwa zilipotiwa wiki mbili zilizopita kuwa,Gazeti la Jambo leo ambalo mwanzo lilimilikiwa na Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania ambapo kwa sasa inadaiwa kuwa kampuni hiyo imeliuzwa Gazeti hilo kwa Kampuni ya Quality Media Group ambayo inamilikiwa na Mwenyekiti wa Klabu ya mpira ya Yanga,Yusuf Manji.
    Mbali na hilo,Gazeti la Raia Tanzania pia nalo limeuzwa pia kutoka kwa Bodi ya wanahisa wa Gazeti la Raia Mwema ambapo kwa sasa Bodi hiyo imeliuza Gazeti hilo kwa Kampuni ya TSN supermarket,inadaiwa sababu ya Bodi ya wamiliki wa Raia Tanzania kuliiuza gazeti hilo baada ya kuporomoka kimauzo.
“Ninachokwambia magazeti haya lazima yafungiwe ndugu,maana yamekiuka sheria ya magazeti ambayo inawataka walete taarifa ofisi ya msajili,lakini hawa hajafanya hivyo ,tena wameikosesha mapato serikali maana wanauziana magazeti kinyemela huku serikali haipati mapato,nakuhakikishia lazima yafungiwe tu.”kimesema chanzo chetu kilichopo ndani ya ofisi ya msajili wa Magazeti.
     Kuibuka kwa taarifa hizi kunakuja ikiwa ni miezi mine tangu uchaguzi mkuu kumalizika ,ambapo Magazeti haya yote  katika kipindi cha Kampeni yalikuwa yanatumika katika kueneza sera za kipropaganda kwa kumbeba alikuwa Mgombea wa Urais kupitia chama cha mapinduzi CCM,John Magufuli na kumshambulia –
Aliyekuwa Mgombea wa Urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendelea Chadema ambaye alikuwa anaungwa mkono na vyama vinavyounda ukawa,Edward Lowassa,kwa kumwandikia makala za kumdhalilisha,
Akizungumza na Fullhabari,blogs,mwandishi wa Gazeti la Raia Tanzania ambaye akutaka kutaja jina lake mtandaoni kwa kuhofia ajira,ameumbia mtandao  kuwa wahariri  wa gazeti lake wamechangia kuliua gazeti hilo,
“Sikufichi bwana,hawa mabwana (Wahariri) wameliua gazeti hili wenyewe,walikubali wenyewe kuiingia kwenye mkenge wa sera za CCM na kuanza kuponda upinzani,wakawagawa wasomaji ndipo Gazeti lilipoingia kwenye msukosuko mpaka wamiliki wakaliuza kwa bei ya kutupwa kwa hawa watu wa TSN,wamejua aliuziki kutokana kuwa alihuziki”

Maoni 1

Bila jina alisema ...

pls fungeni blog ya wananchi pia maana nayo ilizidi