Zinazobamba

NEMC YAWASIHI WAKAZI WA DAR KUHAMA MAENEO HATARISHI YASEMA BOMOA BOMOA IPO PALE PALE,SOMA HAPO KUJUA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhdUy2drD58vs7qRB8bOlwcp5_f-gYHZ5fkwUU74PcQ8_dcEOupdbP6AstdPu6kYlVsDpPG15cgGHECM6WlQ9ZYWpyrvhPn7Sswr3-OwZ2WMSL1i8l_c3u-2BD8RduAXFd6is2TMwzt5kVN/s1600/DSC_0226.JPG
Pichani ni Mkurugenzi wa Baraza la Mazingira (NEMC) Mhandisi Boniventure Baya akizungumza na waandishi wa habari  

SERIKALI yawahimiza wananchi waliojenga makazi kwenye sehemu hatarishi, kingo za mito na maeneo ya wazi kuhama kwa hiyari yao ili kupisha Oparesheni ya bomoa bomoa kuendelea bila kikwazo.
    Hayo yamesemwa na  Mkurugenzi wa Baraza la Mazingira (NEMC) Mhandisi Boniventure Baya wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mhandisi Baya amesema kuwa Serikali itahakikisha haki inatendeka kwa wananchi wote pia itahakikisha haki na usawa wa pande zote wakati wa utekelezaji wa zoezi la bomoabomoa linaloendelea tangu lilipoaza tena Januari 5 mwaka huu.
    Zoezi la bomoabomoa linaendelea jijini Dar es Salaam katika kingo za mto Msimbazi ili kuepusha wananchi kupatwa na madhara mbalimbali ambayo huwa yanakitokeza wakati wa mvua kubwa na masika.
   Mhandisi Baya pia amesema kuwa bonde la mto msimbazi liliainishwa kama ni sehemu hatarishi kwa makazi ya binadamu tangu 1979 na wananchi wa maeneo ya mto huo wakaanza kuvamia kutokana uhaba wa maeneo ya makazi na kuanza kujenga katika kingo za mto huo.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgWjMOXbgw7ECNBHk0VxzJDBzXG8tLAZ64dNRdMwOquoA7F9pG8qZtPho0mPZIvLtXnMyVWRSPIeueKgBAkNZPQ7AgeWoq99Vvj1x9NX1tT1UYZK_dVrdWMvYbRPNli5z27lj7RUF8SiEbA/s1600/DSC_0229.JPG
Pia amewasihi wananchi kutii sheria za ardhi bila shuruti ili kuepukana na madhara mbalimbali yanayojitokeza pamoja na upotevu wa mali zao.

Hakuna maoni