Zinazobamba

MAALIM SEIF AISHIKA MOYO WA ZANZIBAR,KWANI ANAWEZA KUAMUA CHOCHOTE,SOMA HAPO KUJUA

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Shariff Hamad


MGOMBEA urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad ndiye aliyeshika amani ya visiwa vya Zanzibar. Anaandika Faki Sosi … (endelea).
Utulivu wake katika kukabiliana na dhuluma inayotaka kutendwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar ndiko kunakovifanya visiwa hivyo kuwa salama.
Bila shaka, Maalim Seif ikifika mahali akisema ‘liwalo na liwe’ Zanzibar itazama kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hali ya siasa Zanzibar si shwari, wananchi wanaweweseka kutokana na kutokujua kesho yake itakuwaje.
Hatua ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana ndiyo iliyoitumbukiza Zanzibar kwenye mashaka.
Hotuba ya Maalim Seif aliyoitoa juzi jijini Dar es Salaam, inaashiria uvumilivu uliotukuka lakini pia inabeba ujumbe wa kuelekea kuchoka. Si vyema kupuuza hilo.
CCM inagoma kuondoka madarakani, inafanya juhudi kuhakikisha inaendelea kushika hatamu licha ya kukataliwa na Wazanzibari.
Ukweli ulio wazi, Maalimu Seif ametumia nguvu kubwa kuwatuliza wananchi visiwani humo ili kulinda amani na utulivu wa visiwani uliopo sasa.
Kauli ya Maalim Seif kuwataka Wazanzibari kuwa watulivu, inaweza kutafsirika vibaya na makada wa CCM, kauli hiyo haiashirii unyonge hata kidogo.
Maalim Seif wakati mwingine ndivyo alivyo, wakati mwingine huonesha tabasimu hata kama pale jambo analozingumzia kuwa zito.
Namna ilivyo, Wazanzibari wamechoka, subira yao ipo mikononi mwa Maalim Seif, wamechoka kwa sababu wamechoshwa. Hawa wanasubiri kipenga kipulizwe.
Kauli ya Dk. Ali Mohammed Shein ambaye anaendelea mkung’ang’ania madaraka kwamba uchaguzi utarudiwa, inaashiria shari.
Amekiri mbele ya umma kwamba majadiliano yanaendelea lakini hapo hapo anatoa hitimisho kwamba, uchaguzi utarudiwa, Dk. Shein anatangaza ubabe kwamba iwe iwavyo uchaguzi utarudiwa.
Dk. Shein anatangaza uchaguzi kurudiwa huku nyuma ya mgongo wake Jecha akipokea amri. Tafsiri inayochomoka hapa ni kuwa kauli ya Dk. Shein ndio kauli ya Jecha.
Ni vema Dk. Shein akaijali Zanzibar, akathamini uamuzi wa wananchi wake kwamba, zama za CCM zimefika tamati. Kinyume cha hivyo ni umwagaji damu jambo ambalo halipendezi.

Hakuna maoni