Zinazobamba

GAVANA WA BENKI KUU AWAONYA TRA,NI KUHUSU UKUNJAJI REKODI YA UKUSANYAJI WA KODI,SOMA HAPO KUJUA

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa

NA KAROLI VINSENT
Siku moja kupita baada ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kutangaza kuvunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato nchini baada ya kusema wamekusanya trioni 1.4 kwa mwezi Desemba,
        Naye Gavana wa Benki kuu nchini,Profesa Benno Ndulu amewatadhaharisha (TRA) kwa kuwaambiawasizani kiwango hicho walichokusanya kuwa kinaweza kubaki hapo hapo au kuongezeka kwa miezi hii ya mwanzo wa mwaka,
       Kwa madai kuwa miezi ambayo TRA wamekusanya kodi hiyo ni miezi ya mwisho wa mwaka  ambayo makampuni mengi wanatumia miezi hiyo kufanya majumuhisho.
    Akizungumza na waandishi wa habari leo jiji Dar es Salaam,Profesa Ndulu amesema hatua waliyofikia TRA ya kuvunja rekodi ya ukusanyaji kodi ni nzuri ila amesema katika kipindi hiki cha mwenzi wa pili,tatu na wa nne uwenda kiwango cha kodi kikapungua kwa madai miezi hii makampuni hutumia kipindi hichi kujipanga upya.
“Kodi hii tuliyokusanya mwishoni mwaka jana kwa kuvunja rekodi hii tusitegemee tena kama tutakusanya kwa miezi hii ya kwanza kwani makampuni mengi hutumia miezi hii kujipanga upya,kwahiyo uwenda kiwango cha kodi hichi kikapungua au kikabaki hapo hapo”amesema Profesa Ndulu.
Katika hatua Nyengine Profesa Ndulu amesema kitendo cha TRA kuongeza ukusanyaji wa mapato hayo hakitaweza kusaidi thamani ya shilingi yetu kuongezeka thamani huku akitaja njia ambazo zitasaidia thamani ya pesa kitanzania kuongezeka.
Akizitaja njia hiyo ni kuongeza kuuza mauzo nje ya nchi na ili iweze kusaidia kupata pesa nyingi za kigeni jambo analodai ndio njia pekee itakayoweza kuongeza thamani ya fedha yetu,

Hakuna maoni