Zinazobamba

CCM YAANZIMISHA SIKU YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR PEKE YAO,SOMA HAPO KUJUA

Sehemu ya maandamano katika sherehe za Mapinduzi ya 52, wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kibaguzi

MAADHIMISHO ya 52 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yameibua hoja ya mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk, John Pombe Magufuli na Dk. Ali Mohamedi Shein. Anaandika Josephat Isango …. (endelea).
Wakiwa wanaendelea na sherehe hizo zinazofanyika uwanja wa Amani mjini Zanzibar Magufuli aliwasili uwanjani hapo na kuimbiwa wimbo wa taifa pekee.
Alipowasili Rais wa Zanzibar ndiye aliyepigiwa wimbo wa Taifa wa Zanzibar, na mizinga 21 ambayo Magufuli hakupigiwa.
Hoja ya wimbo wa taifa wa Zanzibar huibua dhana ya kuwepo serikali ya bara na ya visiwani ili ya Muungano ndio iwe serikali kuu na ukubwa wa mamlaka kati ya Rais wa Muungano na Rais wa Zanzibar.
Mapinduzi hayo yaliyopambwa na bendera nyingi za CCM, Bendera ya Taifa na Bendera ya Zanzibar yalishereheshwa pia na gwaride la jeshi pamoja na ngoma mbalimbali za asili.
Wageni waliohudhuria katika maadhimisho hayo ni Marais wa wastaafu wa Jamhuri ya Muungano, Ali Hassani Mwinyi, Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete na Rais mstaafu Amani Abeid Karume.
Wengine ni pamoja na Makamu wa Rais mstaafu Dk. Gharib Bilal, Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, Makamu Rais wa sasa Samia Suluhu Hassani na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa.
Aidha hakuna mabalozi wengi waliohudhuria sherehe hizo

Hakuna maoni