WAZIRI MWAKYEMBE AING'ANG'ANIA KATIBA YA SAMWEL SITTA,SOMA HAPO KUJUA
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe
ambaye ameapishwa leo na rais John Magufuli kushika wadhifa huo amewaomba wadau
na wananchi kwa ujumla kumpa muda.
Akiongea na waandishi wa habari muda mfupi baada ya
kuapishwa, Dkt. Mwakyembe ambaye alikuwa waziri wa wizara mbalimbali katika
serikali ya awamu ya nne amesema kuwa anafahamu changamoto nyingi katika mfumo
wa sheria ya nchi akiwa kama mwananchi. Hivyo, ameomba kupewa muda ili
atakapoingia ofisini azifanyie kazi changamoto hizo.
Dk. Mwakyembe ambaye kitaaluma ni mwanasheria
aliyebobea, alieleza kuwa mfumo bora wa sheria ya nchi ni kitu muhimu katika
kipindi hiki ambacho serikali imeamua kufanya mabadiliko makubwa ya kimfumo.
“Tuko katika kipindi cha mageuzi makubwa ya uchumi
wetu na masuala ya kijamii na kiuchumi, kwahiyo masuala ya kisheria
yatajitokeza sana hapo. Ndio maana nasema… sawa ni eneo langu kisheria lakini
changamoto ziko nyingi ambazo lazima tukabiliane nazo ili nchi yetu iende kwa
kasi ambayo rais wetu ameanza nayo,”amesema.
Akizungumzia mchakato wa Katiba Mpya uliokuwa
ukiendelea katika serikali ya awamu ya nne, Dk. Mwakyembe amesema suala hilo
litakamilishwa kutoka pale lilipoishia.
“Mheshiwa rais ameshalielezea vizuri sana hilo
kwamba katika kipindi chake tutalifanyia kazi, na hatukuishia pabaya tuliishia
pazuri tu, tutalitekeleza, muda utafika na naamini tutalikamilisha vizuri
tu,”aliongeza.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni