WAZIRI MPANGO AKABIDHI OFISI TRA,ASEMA YEYE HATA KUWA WAZIRI WA KUOMBA OMBA KWA WAHISANI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt Philip Mpango |
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango amesema
kamwe hata kuwa Waziri ambaye atakuwa omba omba na kuwategemea nchi wahisani.Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hata hivyo,amesema kwa sasa wizara yake kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) watahakikisha wanawawekea
mazingira mazuri wafanyabiashara wakubwa katika kulipa kodi.
Waziri
Mpango ameyasema hayo leo Jijini wakati alipokuwa akikabidhi ofisi aliyokuwa
akihudumu nafasi ya ukaimu Kamishna mkuu wa TRA nchini kwa Kamishna mpya wa
mamlaka hiyo,Alphayo Kidata ambaye awali alikuwa Katibu mkuu Wizara ya
Ardhi,nyumba na Maendeleo na Makazi,
Ambapo
Waziri Mpango amesema nia ya serikali ya awamu ya tanu ni kuhakikisha
inakusanya mapato yake ya ndani kwa kiasi kikubwa na kuondokana na kasumba ya
kutegemea nchi wahisani,
Amesema
kwa sasa amejipanga kuhakikisha anaziba
mianya yote ya ukwepaji kodi ambayo ilikuwa inafanywa na wafanyabiashara
wakubwa ambao walikuwa wanaikosesha mapato serikali kipindi cha nyuma kwa
ukwepaji wa kodi.
Amebainisha
kwa kusema kuwa kwa sasa serikali haita
wabuguzi wafanyabiashara ndogo ndogo kwa kuwakea mazingira magumu ambayo
yalikuwa yanatokana na kodi zisizo za lazima huku akidai kwa sasa serikali ya
awamu ya tano itawaangalia zaidi wafanya biashara wakubwa.
Vilevile,Waziri
Mpango amezitaka taasisi mbalimbali za kibenki kutanua matawi mbalimbali ya
kibenk hadi vijijini ili kuongeza uelewa
akiba zao.
Amesema wananchi wengi waishio vijijini hawana uelewa
wa kutunza pesa katika mabenk na wamekuwa na kasumba ya kutunza pesa
katika maeneo yasiyo stahiki ikiwemo nyumbani
hivyo ameahsa benk zitoe elimu ya
kutosha kwa wananchi ili waweze kuwa na uelewa wa kutunza pesa hizo,
.kutunza
zilizopo nchini kuachana na ukasumba wa sasa wakutegemea mapato yake
ndani ya mijini huku akiwataka kuwakea
Hakuna maoni
Chapisha Maoni