Zinazobamba

UTEUZI WA NDALICHAKO KUWA WAZIRI WA ELIMU WAPINGWA KILA KONA,MAGUFULI AINGIA LAWAMANISOMA HAPO KUJUA

Ujumbe wa Wazi kwa Mheshimiwa John Joseph Pombe Magufuli: Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

KUHUSU DR. NDALICHAKO NA WIZARA YA ELIMU.

Mimi nikiwa kama mdau wa elimu Tanzania na mkerereketwa wa maendeleo ya kweli ya elimu ya nchi hii nina maswala kadhaa ninayojiuliza kuhusu uteuzi wa Dr Ndalikacho kushika nafasi ya uwaziri katika Wizara ya Elimu.

La kwanza ni kuwepo kwa wabunge kadhaa walioteuliwa kihalali na kwa njia ya kidemokrasia na kwa ridhaa ya wananchi, je mheshimiwa Raisi hukupata mtu kutoka huko bungeni mpaka ikafikia kutuletea mtu ambaye si mbunge wa wananchi bali ni mbunge wako? Huku ukizingatia kuwa aliondolewa kusimamia Baraza la Mitihani la Taifa NECTA kutokana na kashfa?

Hivi yale mapungufu yalokuwa yakilalamikiwa na baadhi ya wananchi hadi kupelekea kuondolewa kwake pale NECTA, Mheshimiwa Rasi unataka kutuaminisha kwamba yalikuwa siyo sahihi na kupelekea kumuamini tena kwa kumpatia nafasi kubwa zaidi ya ile ya awali?

Au uteuzi huu ni kumpa nafasi nyingine kuendeleza yale ambayo alikuwa hajayakamilisha wakati alipokuwa NECTA?

Mheshimiwa Raisi, pamoja na kutambua kwetu kuwa ni haki yako kisheria kumteua yeyote na kumpa jukumu lolote lile utakalo, lakini tunaomba ukumbuke kuwa mamlaka hayo umepewa na wananchi, kwa lengo la kuwatumikia katika hali inayokubalika kisheria na kimaadili.

Kumuweka mtu mwenye kashfa na madoa ni kuitia madoa na majipu serikali yako tukufu ambayo inakusudia kusafisha utendaji katika nyanja zote za uma.

Natumai Mheshimiwa Raisi utalitolea maelezo hili la Ndalikacho na ingefaa kama ungemuondoa katika nafasi hiyo.h

Wako

Mdau wa Elimu


Ustadh Ismail S Yusuf

Maoni 21

Bila jina alisema ...

MANENO HAYA YANATISHA LAKINI LISEMWALO LIPO !

Unknown alisema ...

Nnachoamini mm Dr ndalichako ni mtu sahihi kwenye wizara ya elimu! tuhuma na makando kando yote yaliyosemwa na kuundwa juu yake yalikuwa ni ya kisiasa zaidi kwa sababu ya madai ya watu wachache dhidi yake" tuhuma kwa Dr Joyce zilikuwa za kisiasa dhidi ya mtumishi asiye mwanasiasa Bali alikuwa ni mtaaluma' huwezi ukatoa tuhuma za kisiasa na zisiwe na uthibitisho, tuhuma za kisiasa dhidi ya taaluma zinapaswa kujibiwa na kuthibitishwa kitaaluma, hatuwezi kuendelea kwa kuchanganya siasa na taaluma never I say never" ni Nani aliyewahi kuthibitisha tuhuma dhidi ya Dr ndalichako!? na alithibitisha Vp!? je! n kwa ushahidi wa kisiasa, ama kitaaluma!? don't throw stones to Joyce shes the right person no more, namkubali binafsi kwa ushahidi wenye mantiki" tusilete tofauti zetu za kidini na kisiasa ktk hili" taaluma na uzoefu wake ktk elimu vinambeba ktk nafasi hii. full stop

Unknown alisema ...

Huyu ndiye mtu sahihi, alikuwa na tuhuma gani? Aliondolewa baada ya kukataa kupanua magoli ili wanafunzi wapite bila ufaulu. Akaondoe yale magoli na ma GPA yasiyo na tija kwa elimu ya sekondari.

Konki alisema ...

ndalichako ndo mtu sahihi, tunachotaka ni kuzalisha watu walioiva kielimu hata kama ni wachache kuliko kupata wengi ambao hawajiwezi. Ndalichako ondoa mfumo wa GPA na urudishe mfumo wa division

MTEMBEZI HAMAN MTEMBEZI alisema ...

Ndalichako!
Yule yule ninaemfahamu, au mwingine?
Ana kashfa ipi halisi?
Mmh! Watu waliozowea kukopi na kupesti wana matatizo sana, na ndio walioifikisha hapa nchi hii!!
Ndalichako ana tuhuma za watu waliosoma lugha na elimu isiyoweza kuleta tija katika maendeleo ya nchi, iweje asiteuliwe kama mh Dr jpm ameona inafaa?
Mtoa post jipime, nina mashaka na wewe,
Unaweza ukawa na ubinafsi fulani!
Kama angekuwa karibu ndalichako na mh rais ningewpongeza wote juu ya hilo!
Fikiri kabla ya kupost!!

Unknown alisema ...

Huyu ni mtendaji mzuri ni mmoja ya watu au viongozi wenye msimamo wa lile wanaloliamino katika utendaji wake wengi wanaompinga wana masilahi yao binafsi na hao ndio wanaofanya ubora wa elimu yetu iende chini kwa sabau ya kupenda short kati mbalimbali lakini mama huyu alisomamia na aliondoa mkusanyiko mkubwa wa watu kwenda baraza lamitihani kufuata vyeti au huduma mbalimbali kwa kiziweka kwenye mtandao na zidi hakusupport kabisa marekebisho ya kuongeza alama ya ufaulu ya E kabla ya F ambayo pamoja nakuwekwa haibadilishi ufaulu wewe wa mwanafunzi aliyepata hii na wla hawezi endelea na masomo ya juu. Binafsi namkubali sana sana Dr. Ndaichako kwa ni mtu anayeheshimu taaluma nataratibu za kazi yale kwa maislaho mapana ya Taifa badala ya kuwa kwa.kundi fulqno ai taasisi fulani viva ndalichako.

Unknown alisema ...

Nachukiiaaa mpaka nakuwa na kihoro.

babumbwa alisema ...

Ndalichako ndio mtu sahihi kabisa kuiongoza Wizara hiyo, hongera sana Magufuri kwa uteuzi ulioufanya.

Unknown alisema ...

The jembe..... Mtu makini zaidi Joyce ndalichako

Malanilo J. Simon alisema ...

Dr. Ndalichako ni mtu sahihi kwa sababu zifuatazo.
1. Ni msomi aliyebobea katika masuala ya elimu ya Tanzania.
2. Ana uzoefu na mifumo ya elimu nchini Tanzania
3. Ana maono ya kuhakikisha elimu ya Tanzania inakuwa bora. Ndiyo maana JMK alimwondoa katika nafasi yake sababu alikuwa anagomea upanuaji wa magoli kusudi watoto waonekane wanafauru sana wakati ni mbumbu
4. Anatenda haki (wapenda udini hawamtaki dr. Ndalichako kwa sababu zao binafsi)
5. Hapendi ubabaishaji.

Bila jina alisema ...

Ndalichako is the best,mtaaluma asiye babaishwa kisiasa na ataondoa hizo GPA za sekonadari zisizo na maana yoyote kwa hizo levels. nadhani MWISHO WA BRN Umekaribia lazima watu wfauli kwa walichokifanyia kazi haijalishi ni wachache kiasi gani hawaitajiki wanafunzi kufauli huku uwezo sifuri.... Ndalichako hongera mtafiti uliyebobea kwenye masuala ya elimu.
HIYO POST IONDOLEWE TU MAANA HAINA MANTIKI SIYO KILA ALIYECHAGULIWA NA WANANCHI ANASIFA ZA KUONGOZA KWANZA WENGINE TUMEONA WAMEENDA HATA KUPINGWA MAHAKAMANI KWANI HAWAKUSHINDA KIHALALI.
AGAIN NDALICHAKO IS THE BEST MKAWAULIZIE HISRORIA YAKE UDSM IS VERY STRICKY PERSON HANA UBABAISHAJI......

Bila jina alisema ...

NDALICHAKO NI MTU SAHII KABISA KATIKA WIZARA YA ELIMU, AFU HIZO TUHUMA NI ZIP? MBONA HAZIJULIKANI NA WADAU WA ELIMU? walio foji vyeti vya NECTA nadhani wengi hawatakuwa na amani maana JOYCE NDALICHAKO NOW ON AIR,MITAALA ISIYO NA TIJA KWA WANAFUNZI KWISHINEI!!!!!!!

Bila jina alisema ...

Wasifu wa Dk Joyce Ndalichako Elimu 1993 – 1997,Chuo Kikuu cha Alberta, Edmonton, Alberta, Canada; Shahada ya Uzamivu (Ph.D) katika Elimu ya Saikolojia ambako alisomea takwimu, vipimo na tathmini.1987 – 1991, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikosemea Shahada ya Kwanza Elimu akijikita kwenye hesabu na elimu.

Uzoefu wa Kazi Aprili 2015 hadi sasa, Naibu Mkuu wa Kitengo cha Utafiti, Chuo Kikuu cha Aga Khan katika Taasisi ya Maendeleo ya Elimu , Afrika Mashariki. Septemba 2014 hadi sasa, Profesa Mshiriki katika tathmini, Vipimo na Viwango.

Julai 2005– Agosti 2014, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA). 2000 – 2005, Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Agosti - Oktoba 2005 Mshauri Mkuu Mwelekezi katika mpango wa mapitio ya sekta ya elimu.

Desemba 3 – 31, 2004, Mshauri katika mpango wa kuanzisha mafunzo ya Tehama katika vyuo vya ualimu. Januari 14-25, 2004, Mshauri katika mpango wa tathmini katika elimu msingi. Aprili 5-29, 2004, Mshauri katika mpango wa kutathmini utoaji wa elimu katika kambi za wakimbizi nchini . Septemba hadi Oktoba 2003, Mshauri katika mpango wa tathmini ya elimu kwa wote (EFA).

Machi - Mei 2003, Mshauri wa kuendesha mahitaji ya tathmini kwa elimu isiyo rasmi

Bila jina alisema ...

Umenena kweli Mr Stephen, Dr Ndalichako aliondolewa kwa siasa kauzu za Tanzania, otherwise ni mtu sahihi kwa hiyo wizara, watu wanamchukua ni wale wanaopenda elimu mteremko.......... wataisoma namba hamna namna, goo Dr Joyce my prayer will be with you

Unknown alisema ...

Duu ukiona watu wengi wanamkubali mtu furani! na mmoja tu akamtoa kasoro ujue yeye ndiye anakasoro! sasa mm nasema hivi! Mh Joice Ndalichako nenda kafanye kazi na Mh. Raisi amekuchagua kwa maksudi mazima ili Watanzania Waliomchagua kwa shida ya kusota kwenye foleni siku ya uchaguzi na kupigwa na mavumbi kuona wanakuwa na furaha katikat nchi yao. Vilevile suala zima la Elimu jamani ilikuwa issue kubwa! nilikuwa na mengi sana ya kuzungumza hapa ila naona muda sina, ila kifupi Raisi kachagua jembe na tunaimani naye sana Dada Joy! Badilisha Elimu ya Tanzania. Na usiwaonee aibu viongozi ambao utaona watakukwambisha kwenye Wizara nyeti kama hiyo! Tumechoka na kuwa na wahitimu vimeo wa kukopi na kupesti. Be Blessed Madam god will be with you!..


Bila jina alisema ...

Huna akili weww

Bila jina alisema ...

Anzisha serikali yako ndo umtoe Ndalichako

mussa lyimo alisema ...

inategemea watu wa aina gani hupata nakala za gazeti lenu hili ...lakini hakuna lawama zozote anazopewa mtu bila ya kuwepo na sababu ....na tukiangalia hao waliokuja na lawama hizo kimsingi hazitokani kabisa na siasa za nchi bali naweza kusema zinatokana na UDINI ..na huo ni ugomjwa mkubwa uliopo Tanzania kuanzia awamu ya kwanza hadi kuingia katika awamu hii ya tano chini ya Rais Magufuli ambaye sote tunamjua Madhehebu ya dini yake na utumishi wa kanisa lake ...Kwa taarifa zenu Waislaam ndio wamekuwa victims katika nchi hii khasa katika kunyimwa nafasi za Elimu ya juu na kadhalika katika ajira . Tukizingatia takwimu sahihi ya idadi ya wakaazi wa Nchi yetu mutakubaliana kabisa kwammba sense zote zilizofanywa zimebaini kwamba idadi ya waislaam ni kubwa kulinganisha na idadi ya dini nyengine ,,na zipo sababu kadhaa zinazokubalisha takwimu hiyo kukubalika kimaadili /kimazingira na kijamii . Hata hivyo waislaam wa Tanzania nikiwemo na mimi tunajiuliza vijana wa kiislaam wanapoanza shule za msingi wanaonekana wakipata matokeo mazuri kabisa ..lakini hawachaguliwi kuendelea na masomo kwenda sekondari ..ni wachache sana wanaochujwa na kupelekwa sekondari hadi kufikia High School/ Form 6 n.k ...Lakini jambo la kusikitisha ni ule mchujo wa kwenda vyuo vikuu ....ambapo kwa awamu zote tulizozishuhudia ni kuwaona vijana wasiokuwa wakislaam ndio wanaopewa nafasi nyingi za kuendelea na masomo ktk vyuo vikuu na idadi ya waislaam huwa ni ndogo mno mno kiasi cha kuwafanya vijana wa kiislaam waonekane matahira wakifika katika viwango hivyo; Kwa hali hiyo waislaam Nchini wameshayaona hayo na kuyakemea na kuyalalamikia mara kwa mara katika sehemu zote husika lakini hakuna kinachorekebishwa bali ni system ile ile ambayo imekuwa ikubuniwa na kuendelezwa katika wizara hiyo ; na ili lengo na mafanikio ya agenda hiyo ya kuwakwamisha vijana wa kiislaam iendelee na kutumika ...wizara kama hiyo haitowezekana hata mara moja kuongozwa na Muislaam hata akiwa Profesor-kwani katika awamu ya Mzee Mwinyi 1985-1990 kwa bahati mbaya Mzee Mwinyi alimuweka hapo Profesor Malima ambaye aligundua siri kubwa ndani ya wizara hiyo ya ELIMU , na kubaini ujanja na hila zinazotumika za kuwafelesha na kuwakosesha vijana wa kiislaam nafasi za juu za masomo pamoja na juhhudi zao na ubora wao wakiwa madarasani .
Nategemea administrator ataweza kutoa maoni yangu bila ya kinyongo wala chuki ....kwani mara nyingi kuna censorship inayofanyika na baadhi ya editors au wale administrators kwa kuyazuia maoni ambayo kwa upande wao yanawakera; na hili pia litakuwa ni jibu kwa Ndugu yetu Matilda Msekele ambaye anavyoona wengi ya wanaotoa post wanampa support Bi Joyce Ndalichakola bila ya kuweka vipimo vya editing kwa mchujo unaotumika hivi sasa ambapo Uhuru kamili wa kutoa maoni yako unakandamizwa hata na wahariri na administrators wa mitandao ya kijamii kwa maslahi ya ajira zao au dini zao au vyama vyao... Na huo ni ukweli usioweza kabisa kupingika .

HERI alisema ...

sometimes it's wiser to keep quiet if you have nothing to say rather than saying without having enough facts..."WISE PEOPLE SPEAK BECAUSE THEY HAVE SOMETHING TO SPEAK BUT A WISEACRE SPEAKS BECAUSE HE WANTS TO BE HEARD"

Unknown alisema ...

Nimechelewa sana kusoma mawazo ya mlalamikaji kuhusu Profesa Ndalichako.japo nimesoma coments za wachangiaji wawili....kwaharakaharaka naweza kusem huyu mlalamikaji malalamiko yake ni ya kipuuzi kabisa na hana ushahidi.Ndalichako aliomba kupumzika NECTA baada ya kuona viongozi wa kisiasa wanachanganya siasa na Elimu hasa suala la Udivision 5.lakini kuteuliwa kwake na Raisi ni haki ya kisheria.ukisema raisi atue walioko bungeni je kama wote ni la 7 mfano au hawana sifa....wacha upuuzi kabisa Ndalichako is the best for this nahisi umetumwa wewe

Bila jina alisema ...

Anaendelea kudhihirisha kuwa yeye ni mtu sahihi wa nafasi hiyo