NAIBU WAZIRI LUHAGA MPINA AWASHUKIA WATENDAJI NEMC,AWAPA SIKU 30 TU,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI
VINSENT
NAIBU waziri
wa Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina amewapa siku 30 viongozi wa Baraza la Mazingira nchini (NEMC),wawe
wameshatoa hati 512 za wawekezaji waliotaka hati ya mazingira,
Hata hivyo
,amesema endapo agizo hilo lisipotekelezwa basi atamchukulia hatua mkurugenzi
wa NEMC.
Naibu waziri
Mpina ametoa kalipio hilo leo Jijini Dar
es Salaam wakiti alipofanya ziara katika makao mkuu ya NEMC ili kukagua kazi ya
Baraza hilo ambapo amesema inasikitisha kuona wawekezaji wanakosa hati ya
Tasmini ya athari ya Mazingira ambayo inampa ruhusu ya kuwekeza kwenye eneo,
Wanahabari wakimsikiliza Naibu Waziri |
Amefafanua
kuwa Sheria ya Maziringira mwaka 2004 inatoa mda wa siku 30 tu hati hiyo iwe
imetolewa lakini Baraza hilo limetumia siku 90 bila kutoa hati hiyo jambo
analodai kuwa limekuwa likiwakatisha tamaa wakezaji.
“nawapa siku
90 muwe mmetoa hati kwa hawa wawekezaji,naomba kabisa utekelezaji na sitaki kuja
hapa tena nasikia habari hii ya hati,nawaambieni sitokuwa na msamaha
nitamfukuza mkurugenzi ambayo kimamlaka naweza kufanya hivyo”amesema Naibu
Waziri Mpina,
Sanjari na
hayo Mpina amesema kwa sasa wapo mbioni kupeleka marekebisho ya sheria ya
Mazingira ya mwaka 2004 kwa kusema imepitwa na wakati kwani aiendani na wakati
uliopo wamadiliko ya sayansi na teknolojia.
Ameitaja
kasoro katika sheria hiyo ni tozo ndogo unazotoa kwa mtu anayekiuka sheria hiyo
,jambo analodai limechangia watu wengi kupuuza tozi hiyo na kuendelea kuharibu mazingira.
Pichani ni Naibu Waziri akiwa na picha ya pamoja na viongozi wa NEMC |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni