MAMLAKA YA HALI YA HEWA TMA YAZINDUA MFUMO BORA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni mkurugenzi wa TMA,Dkt Agnes Kijazi |
MAMLAKA ya hali hewa nchini (TMA) kwa kushirikiana
na kituo cha kimataifa cha Utafiti kilichopo Marekani “Internation Reseach Institute (IRI) kwa pamoja wamezindua
mfumo utakao wawezesha watumiaji wa huduma
za hizo kuzipata kupitia mtandao wa (TMA).Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akizindua
mfumo huo leo jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti
wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka DktBurahani
Nyezi aliitaka Mamlaka ya hali ya hewa kuongea
ufanisi katika utoaji wa huduma za hali
ya hewa nchini,
Aidha,Dkta
Nyezi ameipongeza TMA kwa jitihada zake za kushirikiana na wataalamu kutoka nchi mbali mbali ambazo ni wanachama wa shirika la hali hewa duniani
katika kuboresha hali hewa nchini,
Vilevile
Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Ushauri TMA aliishukuru kituo cha kimataifa cha (IRI)
kwa msaada waliotia pamoja na kuiwezesha TMA kukamilisha mfumohuo na kufikia
hatua ya kuzinduliwa rasmi,
Kwa upande wake mkurugenzi wa TMA,Dkt Agnes Kijazi alitoa msisitizo kwa wadau
kuzingatia matumizi sahihi ya taarifa za hali hewa ili kuongeza tija na ufanisi
katika shughuli za kiuchumi na kijamii na pia kuweza kukabiliana na
majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni