MAGUFULI AWACHIMBA MKWARA BAKHARESA NA WENZAKE,NI SAKATA LA MAKONTENA BANDARINI,SOMA HAPO KUJUA
Rais John Magufuli akizungumza na wafanyabiashara Ikulu |
RAIS John
Magufuli ametoa siku saba kwa wafanyabiashara walioingiza mizigo yao bila
kulipa kodi wakalipe kwani baada ya hapo watachukuliwa hatua kali za kisheria. Anaandika Erasto Masalu … (endelea).
Hayo yamesemwa leo Ikulu, jijini Dar es Salaam
na Rais Magufuli alipokutana na wadau wa sekta binafsi. Siku hizo sana
zinaanzia leo Desemba 3, 2015.
Mkutano huo wa Rais Magufuli na wafanyabiashara hao ni sehemu ya
kutumika ahadi yake ya kukuza uchumi kupitia kwa kupitia sekta binafsi,
aliyoiahidi wakati wa kampeni zake.
Rais Magufuli amesema katika kipindi cha miaka mitano ya utawala
wake amedhamiria kuijenga nchi na watu wasimuelewe vibaya kwa maamuzi
anayofanya kwani ni kwania njema ya kuleta maendeleo na siyo ujeuri.
Pamoja na hayo Rais Magufuli amewaahidi wadau wasekta binafsi
ushirikiano mkubwa kwani anatambua mchango wao katika kukuza uchumi na pia
amewataka wadau hao kuwa wazalendo na kuliacha kukwepa kulipa kodi ili tuweze
kujenga taifa lenye maendeleo makubwa ya kiuchumi.
Rais Magufuli amewahakikishia wafanyabiashara hao kuwa
watakapokuwa tayari kuwekeza wafanye hivyo kama akikwamishwa na mtu aliyechini
ya uteuzi wake basi mtu huyo ataondoka, kwani sasa ni wakati wa wadau wa sekta
binafsi kuanza kuanzisha viwanda mbalimbali vitakavyotoa ajira.
Pia Rais Magufuli amewapa mawazo ya kibiashara wadau wa sekta
binafsi kuanzisha kampuni ya kutenganisha udongo unaotoka kwenye machimbo ya
madini, kuanzisha viwanda vya samaki pembezoni mwa bahari pamoja na kutengeneza
samani zitokanazo na mazao ya misitu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi
(TPSF), Regnald Mengi amesema kuwa wako tayari kumpa ushirikiano mkubwa rais
katika kuhakikisha uchumi wa Tanzania unakuwa kwa haraka.
Mengi pia amemuomba rais kuendelea kukemea masuala ya rushwa
pamoja kusaidia kupunguza utitiri wa kodi.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni