POLISI YACHARUKA NA WANAOWACHOMA MOTO WEZI NA VIBAKA,YAIBUKA YAJA NA HICHI,SOMA HAPO KUJUA
Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (SSP), Advera Bulimba |
JESHI la Polisi nchini limesema litatoa zawadi nono
kwa mwananchi atayefichua taarifa juu ya watu wanaowashambulia waharifu pindi
wanapowakuta na makosa.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Msemaji
wa Jeshi la Polisi nchini,Advera John Bulimbo wakati wa mkutano na waandishi wa
habari ambapo amesema kwa sasa Jeshi hilo limebaini kuwa kumeibuka juu ya
matukio ya uvunjaji sheria kwa Raia kujichukulia sheria mikononi kwa kupiga
watu wanawaohisi ni waharifu
“Kumeibuka kwa tabia ambayo imejengeka miongoni mwa
jamaii kwa watu kutoheshimu sheria za nchi kwa kujichukulia sheria mkononi kwa
kuwapiga hama kuwachoma moto ama kuwaua
hata kuwadhalilisha kwa watuhumiwa ikiwemo kuwavua nguvu kwa watu wanojihusisha
na vitendo vua uharifu”amesema Bulimba.
Bulimba amesema kuwa jambo hilo ni kinyume na
sheria,kanuni na taratibu za nchi kwa raia yeyote kujichukulia sheria mkononi.
Kufuatia hali hiyo,Bulimba amesema kufuatia hali
hiyo kuongeza mara dufu kwa kipindi hiki,wamewataka wanchi kurekodi tukio
ambalo wapo watu wanafanya uharifu na kuwasilisha ushahidi huo wa video kwa
jeshi la polisi na zawadi nono itatolewa kwa mwananchi atakayefanisha kukamatwa
kwa watu hao wanahojihusisha na tabia hizo.
Kuibuka huko,kwa
Jeshi hilo,kuna kuja ikiwa ni siku kadhaa baada ya matukio ya watu kujichukulia
sheria mkononi kwa waharifu ikiwemo tukio lilotokea mkoani Dar es Salaam na
watu wanaoitwa wenye asira kali kumvamia mwanamke mmoja na kumshabulia kwa
kumpiga mawe kichwani kwa madai anajihusisha na wizi wa Pikipiki.
Ambapo mpaka sasa kwa mujibu wa Takwimu za Jeshi la
Polisi zinasema kwaanzia Januari hadi Octoba ya mwaka huu teyari watu takribani
829 wameripotiwa kuuliwa kutokana na Tabia ya Raia kujichukulia sheria mkononi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni