Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Apiga Marufuku Kuuza na Kunywa Pombe Saa za Kazi
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa amepiga marufuku uuzaji na unywaji wa pombe wakati wa saa za kazi. Amri hiyo ameitoa jana katika taarifa yake aliyoisambaza kwa vyombo vya habari.
Gallawa
alisema kwamba amechukua uamuzi huo kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo
kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya 61, Ibara ndogo ya 4.
Alisema kutokana na amri hiyo itakuwa marufuku kwa wakazi na wafanyabiashara wa mkoa huo kuuza au kunywa pombe kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni.
Alisema kutokana na amri hiyo itakuwa marufuku kwa wakazi na wafanyabiashara wa mkoa huo kuuza au kunywa pombe kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni.
Maoni 1
badala ya kufuatilia mambo ya shule , ujinga , wizi unawazuia wath kupata ulabu ...je kama mimi sifanyi kazi serikalini na niko off na ninataka kupata kinywaji....huu ni ujinga mtupu
Chapisha Maoni