TAASISI ZA ELIMU ZAHIMIZWA KUWATHAMINI WAHITIMU WANAOFANYA VIZURI KATIKA MASOMO YAO.
![]() |
| .Wageni mbalimbali wakitembelea eneo la Vipimo na Mizani wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo na zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo yao katika Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam |
Taasisi za elimu kote nchini zimeaswa kujenga utamaduni wa
kuthamini na kutambua mchango wa wahitimu wanaofanya vizuri katika
masomo yao
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
salaam na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE)
Prof.Emanuel Mjema wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti na zawadi
mbalimbali wahitimu wa chuo hicho takribani 20 waliofanya vizuri katika
masomo yao kwa mwaka 2015.
Akizungumza na
jamii ya wanachuo na Wahitimu wa Zamani wa Chuo cha Elimu ya Biashara na
wale wanaofanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini amesema chuo chake
kina utamaduni wa kuwatuza wahitimu wanaofanya vizuri katika masomo yao
kama motisha kuthamini juhudi zao ili kuhamasisha wengine kufanya
vizuri zaidi.
Amesema wahitimu 20 wa fani
mbalimbali zikiwemo za Rasilimali Watu,Uendeshaji wa Biashara, Ununuzi
na Ugavi, Vipimo na Mizani, Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Masoko na
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ngazi ya Stashahada, Shahada,Diploma
na Cheti wametunukiwa vyeti na kukabidhiwa zawadi mbalimbali.
Prof.
Mjema ameongeza kuwa mbali na tuzo hizo wadau hao hususan wahitimu wa
miaka ya nyuma wa chuo hicho wapata fursa ya kujadili masuala mbalimbali
ikiwemo kukijengea uwezo chuo hicho pamoja na kuangalia shughuli za
kitaaluma zinazofanyika.
" Siku hii ni muhimu
sana kwa Chuo cha Elimu ya Biashara, ni siku ambayo tunathamini wahitimu
wetu waliofanya vizuri kwa kuwapa Zawadi za vtu mbalimbali kuthamini
mchango na heshima waliokipa chuo chuo chetu" Alisisitiza Prof.Mjema.
Ameongeza
kuwa utoaji wa zawadi na tuzo hizo unakwenda sambamba na na maadhimisho
ya ya Mahafali ya 50 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam
yatakayofanyika Novemba 12,2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo
mgeni rasmi atakua Rais mstaafu wa awamu ya Pili Ali Hasani Mwinyi.
Akifafanua
kuhusu mahafali hayo ya 50 amesema kuwa wahitimu wapatao 2050 wa ngazi
mbalimbali watatunukiwa Shahada , Astashahada, Stashahada, shahada na
stashahada za Uzamili.
Kuhusu suala la nidhamu
chuoni hapo hasa mavazi amesema kuwa chuo chake kimeendelea kusisitiza
nidhamu na kuweka kanuni zinazowabana wanafunzi huku akifafanua kuwa
chuo hicho kilikua chuo cha kwanza kuweka sheria inayosimamia nidhamu ya
mavazi kwa wanafunzi.
Amesisitiza kuwa mavazi
ndiyo yanayompambanua mwananfunzi na kuonyesha tabia yake na kuongeza
kuwa nidhamu inapokua juu inawapa wanafunzi fursa nzuri ya kupata ajira
pindi wanapohitimu kwa kuwa tayari wanaaminika katika jamii.
Prof.Mjema
amebainisha hali ya nidhamu ya mavazi inaendelea kuzingatiwa kutokana
na Madhara ya kuzuiwanna kushindwa kuhudhuria vipindi wanayoyapata
wanafunzi waliokuwa wanakiuka kanuni na taratibu za chuo hicho
"Vijana
lazima wawe mfano wa kuiga na hawa ni wasomi ambao wanategemewa na
taifa, CBE imeshafukuza wengi kwa kukosa nidhamu, pia mwanafunzi
anayekosa maadili huathiri maendeleo ya chuo na wanafunzi wengine"
Amesisitiza.
Akizungumza kwa niaba ya wahitimu
wa zamani wa chuo hicho (Alumnae) Bw.Lusekelo Mwandemange amesema kuwa
wao kama wahitimu wanayo dhamana ya kuhakikisha maendeleo ya chuo
hicho yanapatikana.
Amesema wahitimu hao
wamekuwa kioo kwa jamii inayowazunguka kwa kuitumia elimu yao kutatua
changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii
Aidha
wameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuendelea kuweka mazingira
rafiki ya kuwawezesha wanafunzi wa chuo hicho katika fani mbalimbali
kupata elimu yenye viwango ndani na nje ya nchi.
Pia wamesema kuwa wao kama wahitimu wameanzisha umoja wao utakaohusika kuchangia maendeleo ya chuo hicho
Mwisho.





No comments
Post a Comment