UKAWA WACHARUKA WATISHIA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI MKUU,MAUZAUZA YA NEC YATAJWA,SOMA HAPO KUJUA
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi (kulia) akifafanua jambo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Prof. Abdallah Safari |
CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinachoungwa mkono na Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), kimetishia kutoshiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika
Oktoba 25, mwaka huu. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi amesema wanadhamilia kutoshiriki katika
uchaguzi huo kutokana Tume yaTaifa ya Uchaguzi (NEC) kutokuwa na msimamo katika
kazi zake.
Anasema zikiwa
zimebaki siku nne wananchi kuelekea kwenye uchaguzi mkuu lakini NEC hadi sasa
haina msimamo na kuonekana kuyapuuza madai mengi yenye hoja yanayotolewa na
Ukawa.
Akiyataja baadhi
ya madai ambayo NEC imeyapuuza ni kutotoa ushirikiano wa kufafanua juu ya
upigaji kura kwa watu ambao hawakuona majina yao kwenye daftari la kupiga kura
na kutotoa sababu ya utofauti wa namba za kupigia kura kutoka kwenye daftari na
kwenye kitambulisho.
Munisi ameongeza
kuwa, NEC wamepuuza kutoa ufafanuzi juu ya picha ambazo haziitajiki katika
upigaji kura, kutoa ufafanuzi juu ya listi mpya ya wapiga kura iliyosemwa na
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, kwamba kutakuwa na watu wa ziada
ambao hawapo kwenye daftari, Je, wanatoka wapi na wapo wangapi? Amehoji.
“Kwa mtindo huu
ambao NEC inaenda nao wa kukubali watu wasiokuwa kwenye daftari wapige kura na
hata wasiokuwepo kwenye orodha wapige kura mbona hawakutushirikisha sisi wadau
wa uchaguzi? Inaweza kupelekea uvunjifu wa amani. Hilo ndio bao la mkono ambalo
lilisemwa na hatutaki litokee,” amesema Munisi.
Munisi amesema
sababu nyingine kubwa ambayo inaweza kupelekea wasishiriki kwenye uchaguzi ni
kuhusu madudu yaliyopo ndani ya daftari la wapiga kura, ambapo hadi sasa NEC
haijatoa jibu linaloeleweka juu ya makosa ambayo yalionekana kwenye daftari.
Sababu nyingine ya
kutaka kutoshiriki amesema, “Hatuna imani na ujumlishaji wa matokeo ya kura kwa
njia ya mashine zao za kujumlisha kwani zinamapungufu mengi. Tuliomba tume
itumie njia ya kawaida kwa njia ya kalukuleta ili kila mtu alidhike lakini
walidai tunawaingilia kazi zake. Sisi hatutakubali,” amesema Munisi.
Kwa mujibu wa
Munisi amesema, hadi sasa bado wanaendelea na uchunguzi kwenye madaftari ya
wapiga kura ambapo amesema wameshakagua katika mikoa tisa na kubaini matatizo
mengi zaidi yakiwemo ya picha hewa, picha za watu wawili na majina ya kiume
kwenye picha za kike.
“Hapo
hatujafanya katika majimbo yote tulifanya baadhi. Bado tunaendelea na uchunguzi
hadi kesho, tukiona makosa yanazidi kiwango cha kufanya uchaguzi usiende vizuri
basi tunaiomba NEC ipeleke uchaguzi mbele,” amesema Munisi.
Aidha, ameitaka NEC
kutoa orodha maalumu ya vituo vya kupigia kura kwani hadi sasa Ukawa bado
hawajajua idadi kamili ya vituo hivyo wanashindwa kuwaapisha mawakala kwa idadi
ya vituo kubadilishwa kila siku.
Habari hii kwahisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni