MASHEIKH NA MAIMAMU WAMPA KIBANO MAGUFULI NA CCM YAKE,WAIBUA SAKATA LA SHEIKH PONDA,WASEMA MAZITO SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI
VINSENT
WAKATI ikiwa
imebakia siku moja tu kuelekea kwenye siku ya kupiga kura,nayo Kamati ya Masheikh na
Maimamu kutoka mkoa wa Dar es Salaam
wameibuka na kuwataka waislam wote nchini kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga
kura,
Na
kumchagua mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ambaye anaungwa
mkono na vyama vya ukawa, Edward Lowassa kwa kusema ni mtu atakayeleta mabadiriko katika dini ya kiislam nchi.
Tamko hilo limetolewa leo jijini Dar es
Salaam na Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Sheikh Said Omar Rico wakati wa mkutano na
waandishi wa habari ambapo amesema waislam wamechoka na hadaa zinazofanywa na
serikali ya chama cha Mapinduzi CCM ya kuwadanganya kipindi cha uchaguzi na
pindi wakifaniwa kuingia wanawageuka na kuwatesa na kuwanyanyasa viongozi wa
kiislam,
Sheikh Rico huku akiongea kwa uchungu, ameyatolea mfano mateso wanayopata viongozi wa kiislama ni ile alilofanyiwa
mtetezi wa haki za waislam nchini Sheikh Ponda kwa kuendelea kunyanyapaliwa kwa
kunyimwa dhamana,
“Waislam
tunasikitika kwa kitendo cha Sheikh Ponda kuendelea kuwekwa Gerezani kwa
kipindi cha miaka miwili na miezi mitatu sasa bila hata kupata dhamana hali ya
kuwa kesi yake inaruhusu kisheria kupata
dhamana jambo hili tumeona ni hujuma kwetu waislam na tunawaka waislam kutafakari
uharali wa kichagua CCM”amesema Sheikh Rico.
Sanjari na hilo Sheikh Rico amesema hata
kitendo cha Serikali na Jeshi la Polisi
kuendelea kuwafungilia kesi walimu wa madrasa nchini kwa kisingizia na kuwaita
Ugaidi ni sababu ambayo wameitaja ni ishara tosha ya waislam nchini kutafakari
kwa kina na kukataa kuipa kura CCM.
KUHUSU TAMKO LILOTOLEWA NA WATU WANAOJIITA
MASHEHE KUHUSU LOWASSA,
Kamati hiyo ya viongozi hao wa kiroho
wamesikitishwa na tamko lilotolewa na watu wanaojiita mashehe ambao walitoa
tamko hivi karibuni wakisema hawata
mchagua lowassa kwakuwa anashirikiana na Askofu Gwajima eti kufanya hivyo ni
ishara ya Lowassa ni udini.
Akipinga vikali Tamko hilo ,Shekh Rico
amesema ni jambo la lilojaa uongo kwani Lowassa amekuwa karibu sana na
waislam huku akitolea mfano msaada wa
Lowassa kwa waislam huko mkoani Mwanza pale alipochangia pesa za uanzishwaji kituo cha Redio cha IQRA FM .
“Yaani huu ni uongo wa mchana kwani
Lowassa alipokuwa anachangia redio ya Iqra Fm aliwachangia mchango mkubwa
tu kiasi cha kwamba mashehe hao walimvirisha Lowassa joho na kilemba cha
kumpa jina la Adfdullah je,udini wake hawakuona
wanauona leo kwakuwa yupo UKAWA”Amehoji Shekh Rico.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni